Mgombea
nafasi ya Uenyekiti wa UVCCM kata ya Kawe Amani Nkurlu (kulia)
akirudisha fomu ya kugombea nafasi hiyo kwa Katibu wa UVCCM kata ya Kawe
Bi. Aisha Katundu.
Katibu
wa UVCCM kata ya Kawe Bi. Aisha Katundu (kushoto) akipokea fomu
aliyoijaza Bw. Amani Nkurlu kwa nafasi ya kugombea Uenyekiti UVCCM kata
ya Kawe alipofika ofisini hapo leo saa 7 mchana.
Mgombea
wa Uenyikiti wa UVCCM kata ya Kawe, Amani Nkurlu, akizungumza machache
na Katibu wa CCM Kawe Bi. Aisha Katundu katika ofisi za CCM Kawe.
Amani Nkurlu akijaza fomu ya kugombea nafasi ya Uenyekiti wa UVCCM kata ya Kawe.
Baadhi
ya wakereketwa wa CCM katika picha ya pamoja nje ya ofisi ya CCM Kawe.
Kutoka kushoto ni Katibu Mwenezi wa tawi la Umbwelani Kawe- Ramadhani
Malenge, Katibu wa Wazazi Kawe- mama Katenda, mgombea nafasi ya ukatibu
UVCCM kata ya Kawe – Sambili Tegemeo na mgombea nafasi ya Uenyekiti
UVCCM kata ya Kawe – Amani Nkurlu.Picha na Josephat Lukaza
Baada
ya uchaguzi wa UVCCM katika kata la Kawe kuvurugika mapema mwaka huu,
uchaguzi huo unaorudiwa sasa umefika patamu ikibakia siku moja tu
kuchukua fomu huku vijana wengi wakijitokeza kuwania nafasi mbali mbali
katika jumuiya hiyo ya vijana illiyopo wilayani Kinondoni.
Akizungumza
na waandishi wa habari, mmoja wa wagombea wa Uenyekiti wa UVCCM katika
kata hiyo, Amani Nkurlu (23) alisema “Siku zote nimekuwa nikitafakari ni
kwa namna gani nitaweza kutoa mchango wangu katika chama na kuchangia
mustakabali wa taifa letu Tanzania kwa ujumla.”
“Ninaamini
CCM bado inahitaji vijana makini na wengi zaidi wakukisemea, kuishauri
na kuleta chachu ya maendeleo katika utendaji wake wa kazi wa kila siku
kichama na kiserikali. Hii ndio dira yangu kwa CCM, nina imani na chama
changu na nimejikita katika kuchangia mabadiliko hayo kupitia Umoja wa
Vjiana,” Nkurlu alisema.
Nkurlu
ambaye ana Shahada ya Mawasiliano kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu
Agustino (SAUT) ameshawahi kushika nyadhifa mbali mbali za uongozi
ukiwemo; Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM – Tawi maalum la Kambarage SAUT,
Waziri wa Mambo ya Nje, Mbunge katika serikali ya wanafunzi, na Rais wa
AIESEC akiwa hapo hapo chuoni. Mwaka 2010 Nkurlu pia alipata kugombea
nafasi ya Umakamu wa Rais katika serikali ya wanafunzi chuoni hapo
lakini hakufanikiwa kwa kupata kura 1278 kati ya kura 2995 zilizopigwa
na 54 kuharibika.
Hivi
sasa Nkurlu anamalizia Stashahada ya juu kutoka Chuo cha Diplomasia na
pia ni mwajiriwa katika moja ya makampuni ya mawasiliano na matangazo
jijini Dar es Salaam kama Mshauri wa Mawasiliano.
No comments:
Post a Comment