*Ahimiza matumizi ya vyandarua kujikinga na malaria
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda
amewataka Watanzania wote kushiriki chanjo ya kuzuia kichomi na kuhara
kwa watoto pindi itakapoanza kutolewa mapema mwakani.
Ametoa wito huo wakati akizungumza na maelfu ya wakazi wa
kata ya Kibaoni na kata jirani za Ikuba, Usevya, Mbede, Mamba na
Majimoto walioshiriki kula naye chakula cha mchana kuadhimisha sikukuu
ya Krismasi.
Sherehe hizo zilifanyika kwenye
uwanja wa shule ya msingi Kakuni ambako pia ni kijijini kwake kata ya
Kibaoni, wilayani Mlele, mkoani Katavi.
“Serikali itaanza kutoa chanjo ya kuzuia kichomi (kitaalam wanaiita pneumonia)
na ya kuzuia kuhara. Magonjwa haya mawili yana madhara makubwa kwa
watoto wadogo. Natoa wito kwa Watanzania wake kwa waume, wakati ukifika
wapelekeni watoto kwenye hiyo chanjo ili kuokoa maisha yao,”
alisisitiza.
Alitumia fursa hiyo kuwahimiza
wakazi wa kata hizo kununua vyandarua na kuvitumia ili kujikinga na
ugonjwa wa malaria kwa vile ndiyo unaoongoza kwa vifo nchini kuliko
magonjwa mengine.
“Nawasihi wafugaji, ninyi mna
hela… uzeni mifugo ili mpate fedha ya kununua chandarua, takwimu
zinaonyesha kuwa kila baada ya dakika tano kuna mgonjwa anakufa kutokana
na malaria. Kwa hiyo mtu akipata visenti vyake, anunue chandarua kwa
mkewe na watoto,” alisisitiza.
Akizungumzia kuhusu UKIMWI,
Waziri Mkuu alitaka wakazi wa jimbo lake la Katavi kutambua kwamba
ugonjwa huo upo na kwamba hauna tiba na tena hauchagui kijana wala mzee,
kijana wa kiume au wa kike.
No comments:
Post a Comment