MUUNGANO wa Makanisa nchini
unatarajia kufanya Mkesha wa kuliombea Taifa ili amani na utulivu uliopo
uweze kudumu, ambao unatarajiwa kufanyika Desemba 31 mwaka huu kwenye
viwanja vya Taifa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na wandishi wa habari
jijini Dar es Salaam leo, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi, Godfrey
Malassy , alisema mkesha huo umekuwa ukifanyika kila Desemba 31 ya kila
mwaka, kuukaribisha mwaka mpya.
Alisema lengo la mkesha huo ni
kuliombea Taifa hilo mungu, ili aweze kuliponya na kulinusuru na majanga
mbalimbali, na kudumisha amani miongoni mwa jamii yote nchini.
Malassy aliongeza kuwa Taifa kwa
sasa linapita katika kipindi kigumu hususani kuanzia uelewa, uchumi, na
katika masuala ya usalama wa raia wa ndani na nje ya nchi ambapo kuna
baadhi ya watu wameanza kuichezea amani kwa kusababisha vurugu kwa
kvisingizio vya dini.
Pia alisema kuwa Watanzania
wanapaswa kudumisha amani na utulivu kwani hiyo ni tunu ambaayo
wamepatiwa na mungu hivyo haipaswi kuchezewa na watu wachache wasio na
nia njema.
“Mkesha wa dua hilo, utafanyika
Desemba 31 mwaka huu kuanzia saa 2:00 usiku hadi asubuhi katika viwanja
vya Taifa Dar es Salaam, na tunatarajia Rais Jakaya Kikwete atakuwa
mmoja wa wageni wetu waalikwa” alisema Malassy.
Malassy alibainisha kuwa mkesha
huo wa maombezi utashirikisha mikoa zaidi ya 16 ya Tanzania Bra na
Visiwani, ambapo utakuwa na lengo la kuwaleta Watanzania kuliombea Taifa
kwa ajili ya kudumisha amani, umoja na mshikamano visitetereke.
No comments:
Post a Comment