Na Ali Issa, MAELEZO-ZANZIBAR
WILAYA YA KASKAZINI A
MAWAKALA
1,500 kutoka vyama mbalimbali vya siasa kutoka majimbo manne ya Mkoa wa
Kaskazini Unguja, wamepatiwa mafunzo ya usimamizi wa uchaguzi wa
marudio wa Zanzibar, unaotarajiwa kufanyika Machi 20, mwaka huu.
Mafunzo
hayo yametolewa leo katika skuli ya msingi Mahonda, yakishirikisha
mawakala kutoka majimbo ya Donge, Mahonda, Bumbwini na
Kiwengwa.Akifungua mafunzo hayo, Msimamizi Mkuu wa uchaguzi Wilaya ya
Kaskazini ‘B’ Makame Khamis Pandu, amesema lengo la Tume ya Uchaguzi
Zanzibar kutoa mafunzo hayo, ni kuwawezesha kutekeleza majukumu yao
katika kufanikisha uchaguzi huo.
Aidha
alifahamisha kuwa, uwakilishi mzuri wa vyama vyao ndio utakaosaidia
kuendesha uchaguzi usiokuwa na mivutano na hivyo kuendeleza amani na
utulivu nchini.“Mafunzo haya ni muhimu kwenu kwani nyinyi ndio
mnaotegemewa na vyama vyenu katika kuviwakilisha na kuhakikisha zoezi la
kusebu kura linafanyika kwa uwazi pasi na matatizo yoyote,” alieleza
Pandu.
Msimamizi
huyo alisema wakala wa vyama vya siasa hapa Zanzibar wapo kwa mujibu wa
sheria ya Tume ya Uchaguzi na ushiriki wao ni muhimu katika kufanikisha
zoezi hilo na kuondoa kasoro zinazoweza kujitokeza.
Mafunzo
hayo ya siku moja ni miongoni mwa hatua za tume kuwapa elimu wadau wote
wa uchaguzi wakiwemo makarani wataobahatika kuteuliwa kwa ajili ya
shughuli hiyo muhimu ya kutafuta Rais na viongozi wa majimbo.
Kwa
hivyo, aliwataka mawakala hao kuyapokea vyema mafunzo hayo na kasha
wakayafanyie kazi kwa manufaa ya taifa.Washiriki wa mafunzo hayo
walihakikisha kwamba watayafanyia kazi maelekezo yote na kuwajibika kwa
mujibu wa sheria ya uchaguzi.
IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR-