TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, June 28, 2013

MASHABIKI SIMBA WAJAZANA KUISHUHUDIA TIMU YAO KINESI DAR ES SALAAM.

 Mashabiki wa Timu ya Soka ya Simba ya Jijini Dar es Salaam, wakifuatilia kwa Makini Mazoezi ya Timu hiyo wakati wa Usaili wa Wachezi na Maandalizi ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara katika Uwanja wa Kinesi Dar es Salaam
 Mashabiki wa Timu ya Soka ya Simba ya Jijini Dar es Salaam, wakifuatilia kwa Makini Mazoezi ya Timu hiyo wakati wa Usaili wa Wachezi na Maandalizi ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara katika Uwanja wa Kinesi Dar es Salaam
 Basi la abiria Daladala linalofanya kazi ya Usafirishaji Ubungo Mbezi, likiwa katika hali ya kusababisha msongamano wa magari eneo la Kimara kutokana na Kuishiwa Mafuta wakiwa katika mzunguko wa kusafirisha abiri, kitendo ambacho pia kilikuwa kero kwa abiria waliokuwa wakiwahi makazini, hali ambayo pia usababisha Ajali kutokana na kuharibikia katikati ya barabara.
 Washiriki wa Mashindano ya Miss Inter University Dar es Salaam, wakiwa katika mazoezi ya katika Ukumbi wa Sansiro Dar es Salaam leo kujiwinda na Onyesho litakalofanyika kesho(Leo) katika Ukumbi huo wa Sansiro, washindi wataungana na washindi wa kanda zingine kuunda kikosi cha Tanzania katika mashindano ya Vyuo Vikuu Tanzania(Tanzania ambassador of Democracy 2013)
 Wachezaji wa Timu ya Soka ya Simba wakipanga mipira katika Moja ya Mazoezi ya Kupiga Mashuti, kwenye mazoezi ya timu hiyo katika uwanja wa Kinesi Dar es Salaam leo
 Wachezaji wa Timu ya Soka ya Simba wakipanga mipira katika Moja ya Mazoezi ya Kupiga Mashuti, kwenye mazoezi ya timu hiyo katika uwanja wa Kinesi Dar es Salaam leo
Washiriki wa Mashindano ya Miss Inter University Dar es Salaam, wakiwa katika Pozi  wakati wa mazoezi katika Ukumbi wa Sansiro Dar es Salaam leo kujiwinda na Onyesho litakalofanyika june 29 katika Ukumbi huo wa Sansiro, washindi wataungana na washindi wa kanda zingine kuunda kikosi cha Tanzania katika mashindano ya Vyuo Vikuu Tanzania(Tanzania ambassador of Democracy 2013).

Wednesday, June 26, 2013

Club Sansiro kukamata Inter city jumamosi 29 mwezi huu

Club Sansiro imeandaa Onyesho la Urembo Miss Inter  university 2013 itakayofanyika katika Ukumbi wa Sansiro kuanzia majira ya saa mbili Usiku na kuendelea, Shindano hili la Vyuo Vikuu ni Mwendelezo wa Mashindano mengine ambayo tayari yamefanyika katika mijin ya Dodoma na Mwanza mapema mwishoni mwa Mwezi May.

Akizungumzia Maandalizi Mwandaaji wa Mkoa wa Dar es Salaam, Fredy Kimiti amesema kwamba shindano hili katika mkoa wa Dar ni changamoto ambayo itaanza mapema kwa wanafunzi wa Vyuo vya jiji la Dar es Salaam kushindana katika Mbio(Riadha) kwa wanaume na wanawake.

na kwamba mashindano kwa upande wa Riadha yataanza Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam kuelekea Leaders Club ambako pia kutakuwapo na Changamoto ingine ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Kutimuana katika Mchezo wa Mpira wa MIGUU.

Washindi wote katika Sanaa hizo wataungana na Washindi wengine kutoka kanda zote za Tanzania katika kinyang'anyiro cha kuwasaka washindi wa Taifa wa Vyuo Vikuu katika Riadha, Soka na Urembo.

MASHAUZI CLASSIC KUIZINDUA NAWINA RESORT MBAGALA KUU

Bendi ya Mashauzi Classic chini ya I sha Mashauzi imeandaa Uzinduzi Rasmi wa Ukumbi wa Nawina Resort Mbagala kuu baada ya Matengenezo kutokana na ajali ya moto iliyotokea mwanzoni
mwa mwaka huu.
akizungumzia Uzinduzi huo mkurugenzi wa Nawina Resort Marry Komba, amesema kwamba Matayarisho yamekamilika na Tayari Isha Mashauzi na Kundi lake wamekamilisha taratibu zote kuhusiana na Onyesho hilo la Uzinduzi siku ya jumamosi tarehe 29 mwezi huu.
"Kikubwa ninamshukuru Mungu kwa kuwezesha kukamilika kwa Ukumbi huu wa Nawina Resort, kama unavyojulikana ukumbi huu na wakazi wengi wa Mbagala Kuu, ndiyo pekee uliokuwa ukiwapatia burudani mbalimbali wakazi wa maeneo haya a Vitongoji vyake vyote, kwa hiyo nawaomba wakazi wa mbagala Kuu waendelee kuunga mkono juhudi hizi ambazo ni kiburudisho kwao, nachukua fulsa hii kuwakaribisha sana siku ya Ufunguzi ili waweze kufika kushuhudia Nawina Mpya chini ya Mashauzi Classic" alisema Marry Komba
Awali kabla ukumbi wa Nawina Resort aujaungua Moto, ulikuwa ni kati ya Miimili ya Burudani iliyokuwa ikiwapa raha wakazi mbalimbali wa Mbagala, ikiwa ni pamoja na Miziki ya Kizazi kipya, Miziki ya Bendi, Taarabu na hata vikundi vya Sanaa kutoka kwa wasanii mbalimbali hapa nchini.
kwa Upande wake Isha Ramadhani maaufu kama Isha Mashauzi amesema kwamba wamejipanga kufanya Onyesho kali na la kusisimua ambapo wakazi wa Mbagala Kuu na Vitongoji vyake wafike ili waweze kufurahia Burudani kutoka katika kundi lake," Nimejipanga vizuri kuhakikisha wakazi na wapenzi wangu tunafanya kitu kipya na siku hiyo nitawapa pia vitu vipya kwa kuwa ni siku ya Ufunguzi wa Ukumbi Mpya, maana hivi sasa Nawina ni mpya kwa hiyo tutaingia na nyimbo zingine mpya ambazo ni burudani ya kupendeza" alisema Isha Mashauzi
katika onyesho hilo ambalo linatarajia kuanza majira ya saa mbili za Usiku , kiingilia  kimewekwa cha kuridhisha ili kuwafanya wakazi wote wa mbagala kufika ili kupata burudani wakiwa nafamilia zao kwa shilingi 5000 tu.
Kuhusiana na Ulnzi wa mali za wote watakaofika, Usalama wa vyombo vya Usafiri , mkurugenzi wa Nawina Resort  Marr Komba alisema kuwa ulinzi ni wa kutosha kwa wote watakaofika siku hiyo.

Monday, June 24, 2013

Mechi Dhidi Ya Ivory Coast Yaingiza Mil 500/-


Mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia, Kundi C, Kanda ya Afrika kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Ivory Coast (The Elephants) iliyochezwa jana (Juni 16 mwaka huu) imeingiza sh. 502,131,000 kutokana na watazamaji 57,203.
Tiketi za kushuhudia mechi hiyo ziliuzwa kwa sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 30,000.
Mgawanyo wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ni sh. 76,596,254.24 wakati wa gharama za uchapaji tiketi ni sh. 7,809,104.
Asilimia 15 ya uwanja sh. 62,658,846.26, asilimia 20 ya gharama za mechi sh. 83,545,128.35 na asilimia 5 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 20,886,282.09.
Asilimia 60 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 250,635,385.06 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 12,531,769.25 ambayo ni asilimia 5 kutoka kwenye mgawo wa TFF.
Mechi iliyopita ya Stars dhidi ya Morocco (Lions of the Atlas) kwenye uwanja huo iliingiza sh. 226,546,000.