Bendi ya Mashauzi Classic chini ya I sha
Mashauzi imeandaa Uzinduzi Rasmi wa Ukumbi wa Nawina Resort Mbagala kuu
baada ya Matengenezo kutokana na ajali ya moto iliyotokea mwanzoni
mwa
mwaka huu.
akizungumzia
Uzinduzi huo mkurugenzi wa Nawina Resort Marry Komba, amesema kwamba
Matayarisho yamekamilika na Tayari Isha Mashauzi na Kundi lake
wamekamilisha taratibu zote kuhusiana na Onyesho hilo la Uzinduzi siku
ya jumamosi tarehe 29 mwezi huu.
"Kikubwa
ninamshukuru Mungu kwa kuwezesha kukamilika kwa Ukumbi huu wa Nawina
Resort, kama unavyojulikana ukumbi huu na wakazi wengi wa Mbagala Kuu,
ndiyo pekee uliokuwa ukiwapatia burudani mbalimbali wakazi wa maeneo
haya a Vitongoji vyake vyote, kwa hiyo nawaomba wakazi wa mbagala Kuu
waendelee kuunga mkono juhudi hizi ambazo ni kiburudisho kwao, nachukua
fulsa hii kuwakaribisha sana siku ya Ufunguzi ili waweze kufika
kushuhudia Nawina Mpya chini ya Mashauzi Classic" alisema Marry Komba
Awali
kabla ukumbi wa Nawina Resort aujaungua Moto, ulikuwa ni kati ya Miimili
ya Burudani iliyokuwa ikiwapa raha wakazi mbalimbali wa Mbagala, ikiwa
ni pamoja na Miziki ya Kizazi kipya, Miziki ya Bendi, Taarabu na hata
vikundi vya Sanaa kutoka kwa wasanii mbalimbali hapa nchini.
kwa
Upande wake Isha Ramadhani maaufu kama Isha Mashauzi amesema kwamba
wamejipanga kufanya Onyesho kali na la kusisimua ambapo wakazi wa
Mbagala Kuu na Vitongoji vyake wafike ili waweze kufurahia Burudani
kutoka katika kundi lake," Nimejipanga vizuri kuhakikisha wakazi na
wapenzi wangu tunafanya kitu kipya na siku hiyo nitawapa pia vitu vipya
kwa kuwa ni siku ya Ufunguzi wa Ukumbi Mpya, maana hivi sasa Nawina ni
mpya kwa hiyo tutaingia na nyimbo zingine mpya ambazo ni burudani ya
kupendeza" alisema Isha Mashauzi
katika
onyesho hilo ambalo linatarajia kuanza majira ya saa mbili za Usiku ,
kiingilia kimewekwa cha kuridhisha ili kuwafanya wakazi wote wa mbagala
kufika ili kupata burudani wakiwa nafamilia zao kwa shilingi 5000 tu.
Kuhusiana
na Ulnzi wa mali za wote watakaofika, Usalama wa vyombo vya Usafiri ,
mkurugenzi wa Nawina Resort Marr Komba alisema kuwa ulinzi ni wa
kutosha kwa wote watakaofika siku hiyo.
No comments:
Post a Comment