Miss Tanzania namba mbili 2006, mwanamitindo na mcheza
filamu, Jokate Mwegello, akicheza na mmoja wa watoto wanaolelewa katika
Kituo cha Yatima cha Extrem cha Tandale kwa Bi Mwamvua Jumanne,
alipotembelea kuwapa zawadi ya Sikukuu ya Krismas na Mwaka Mpya. Zawadi
alizotoa ni mchele, unga wa sembe, sabuni na ndala zenye nembo za
Kidoti. Picha na Jumanne Juma
Miss Tanzania namba mbili 2006,
mwanamitindo na mcheza filamu, Jokate Mwegello, akimpa zawadi ya ndala
mmoja wa watoto wanaolelewa katika Kituo cha Yatima cha Extrem cha
Tandale kwa Bi Mwamvua Jumanne, alipotembelea kuwapa zawadi ya Sikukuu
ya Krismas na Mwaka Mpya. Zawadi alizotoa ni mchele, unga wa sembe,
sabuni na ndala zenye nembo za Kidoti. Picha na Jumanne Juma
Miss Tanzania namba mbili 2006,
mwanamitindo na mcheza filamu, Jokate Mwegello, akiwa katika picha ya
pamoja na watoto wanaolelewa katika Kituo cha Yatima cha Extrem cha
Tandale kwa Bi Mwamvua Jumanne, alipotembelea kuwapa zawadi ya Sikukuu
ya Krismas na Mwaka Mpya. Zawadi alizotoa ni mchele, unga wa sembe,
sabuni na ndala zenye nembo za Kidoti. Picha na Jumanne Juma
………………………………………………………………………….
MISS Tanzania namba mbili 2006,
mbunifu mavazi na muigizaji wa filamu za kibongo, Jokate Mwegelo
‘Kidoti’, jana ilitoa msaada wa vitu mbalimbali katika Kituo cha Kulea
Yatima cha Extrem kilichopo Tandare kwa Bi Mtumwa, Kinondoni, jijini
Dar es Salaam.
Mrembo huyo ambaye pia ni
mkurugenzi wa kampuni ya Kidoti inayojihusisha na masuala ya urembo,
alitoa msaada huo kama zawadi yake ya Sikukuu ya Krismas na Mwaka Mpya
kwa watoto hao kama sehemu ya kuwafariji ili nao kujiona wako sawa na
wengineo wanaioshi nawazazi wao.
Akizungumza mara baada ya
kukabidhi msaada huo, Jokate alisema kuwa ameguswa na kituo hicho
ambacho huwa hakikumbukwi na wahisani kutokana na mazingira ya eneo
hilo.
“Nimefika hapa kutoa msaada kama
sehemu ya kuonyesha ninavyoguswa na jamii ya watoto kama hawa, lakini
pia nikiwa na lengo la kuwafariji ili nao kujiona ni sehemu ya jamii ya
Watanzania,” alisema.
Kidoti alitumia fursa hiyo kutoa
wito kwa watu wenye uwezo, kampuni na taasisi mbalimbali kuona umuhimu
wa kusaidia makundi hayo maalumu katika jamii kwani nao wana haki ya
kuishi na kufurahia maisha kama wengine.
Msaada aliokabidhi kwa
ushirikiano na kampuni ya Raibow Shell, ni mchele, unga wa sembe,
sabuni, jozi za viatu vyenye nembo za Kidoti.
Akizungumza baada ya kupokea
msaada huo, mlezi wa watoto hao, Mwamvua Jumanne, alitoa pongezi kwa
Kidoti na kuwasihi wengine kuiga mfano wa mrembo huyo kusaidia makundi
maalum.
Akielezea changamoto zilizopo
katika kituo hicho, Mwamvua alisema ni kukosa uwezo wa kifedha kuwalipia
ada watoto wanaosoma elimu ya msingi na sekondari, gharama za matibabu
pamoja na kukosa watu wa kuwatembelea ili kuwafariji.