Kiungo-mshambuliaji wa timu ya
makipa Tanzania (TAGA), Deogratius “Dida” Munishi akiwania mpira na
mshambuliaji wa Taswa FC, Ibrahim “Maestro” Masoud katika mchezo maalumu
wa kirafiki uliofanyika kwenye uwanja wa Bora kijitonyama. TAGA FC
ilishinda kwa mabao 3-0.
Mshambuliaji wa timu ya chama
cha makipa Tanzania (TAGA), Ivo Mapunda akimiliki mpira na kiungo wa
Taswa FC, Martin Peter katika mchezo maalumu wa kirafiki uliofanyika
kwenye uwanja wa Bora kijitonyama. TAGA FC ilishinda kwa mabao 3-0.
…………………………………………………………………
Na Mwandishi wetu
Timu ya soka ya Chama Cha
Magolikipa Tanzania (TAGA) imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya
Timu ya soka ya waandishi wa habari za Michezo nchini (Taswa FC) katika
mchezo maalum wa kirafiki uliofanyika kwenye uwanja wa Bora, Kijitonyama
jijini.
Mchezo huo maalum awali
ulitakiwa kufanyika kwenye uwanja wa Karume, ulihamishiwa uwanja wa
bora kutokana na ‘Mizengwe’ ya dakika za mwisho ya wamiliki wa uwanja
huo.
Timu zote zilianza mchezo huo
kwa kasi na kukosa nafasi kadhaa za wazi. TAGA ndio ilikuwa ya kwanza
kulifikia lango la Taswa FC ambayo ilizindua jezi zake kwa mara ya
kwanza zilizotolewa na Benki ya Posta Tanzania (TPB), hata hivyo
mshambuliaji wake, Ivo Mapunda akipiga nje.
Makipa walikuwa katika nafasi
nzuri ya kufunga tena katika dakika ya sita ya mchezo, hata hivyo penati
ya Shaaban Kado ikipanguliwa na kipa wa Taswa, Ahmed Famau.
Taswa FC iliibuka katika dakika
ya nane ya mchezo na Zahoro Mlanzi alikosa bao la wazi akiwa na kipa wa
TAGA FC, Fatuma Omari ambaye pia alifanya kazi ya ziada kuokoa mipira
miwili ya kona iliyokuwa ikiingia wavuni kutoka kwa Majuto Omary.
Makipa walitumia mazoezi yao ya
kila siku vizuri na kupata bao katika dakika ya 14 lilolofungwa na
Mapunda kufuatia krosi safi ya Saleh Malande alicheza vizuri na Juma
Kaseja na Ali “Barthez” Mustapha ambaye pia alifunga bao la tatu. Bao la
pili la makipa lilifungwa na Shaaban Kado baada ya kazi nzuri ya
Deogratius “Dida” Munishi.
Rais wa makipa hao, Alex
Ndembeka alisema kuwa wamefarijika sana mchezo huo ambao umetumika rasmi
kuzindua chama chao ambacho lengo lake kubwa ni kuendeleza fani hiyo
kwa kuvumbua vipaji na kuondoa fikra za kuwa ‘magolikipa’ hawapendani.
“Tunawapongeza waandishi kwa
kukubali wito wetu na kufanikisha kuzindua chama hiki, nadhani umeona
jinsi ilivyo kwa makipa wetu kucheza pamoja, kufurahi na kuondoa mtazamo
hasi wa kuwa makipa hawapendani,” alisema Ndembeka.
No comments:
Post a Comment