Polisi
wa kimataifa , interpol tawi la Tanzania wamemkamata mfanya biashara
maarufu raia wa Kenya kwa tuhuma za kujihusisha na ujangili na uhalifu
uliovuka mipaka ,hususan mauaji ya tembo .
mtuhumiwa huyo Mohamed
Ally Feisal Amekamatwa mjini Dar-Es-Salaam baada ya kusakwa kwa kipindi
kirefu kwa makosa hayo ya kimataifa kutoka Dar Regina Mziwanda anaarifu
zaidi.
Akitbibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo Bwana Diwani
Athumani kutoka kamisheni ya Kurugenzi ya makos aya jinai amesema
mtuhumiwa huyo anakabiliwa na tuhuma za kujihusisha na vitendo vya
uhalifu wa kimataifa ikiwemo uwindaji wa uliovuka mipaka kimataifa
katika nchi mbali mbali)
Bwana Athumani Diwani alieleza kuwa kwa
sasa mtuhumiwa huyo anashikiliwa huku upelelezi ukiendelea kujua makosa
mengine aliyoyafanya kuhusiana na biashara za bidhaa zitokanazo na Tembo
ndani ya Tanzania na katika nchi nyingine za Afrika Mashariki ikiwemo
nchi yake ya asili Kenya.
Mohamed Feisal Ally amekuwa akitafutwa
kwa muda mrefu kwa tuhuma za uwindaji haramu husani mauaji ya Tembo
tatizo ambalo ni kubwa hususani katika ukanda huu wa Afrika Mashariki
hasa Kenya na Tanzania ambapo idadi kubwa ya Tembo wamekuwa wakiuawa
kila mwaka na kutishia kutoweka kwa viumbe hao.
No comments:
Post a Comment