Na: BBC SWAHILI
Bunge la Somalia limeidhinisha uteuzi wa waziri mkuu mpya akiwa ni afisa wa tatu kuhudumu katika wadhfa huo katika kipindi cha miaka miwili.
Bunge la Somalia limeidhinisha uteuzi wa waziri mkuu mpya akiwa ni afisa wa tatu kuhudumu katika wadhfa huo katika kipindi cha miaka miwili.
Wengi wa wabunge walimpigia kura Omar Ali Sharmarke.
Mapema
mwezi huu walipitisha mswada wa kutokuwa na imani dhidi ya aliyekuwa
waziri mkuu Abdiweli Sheikh Ahmed,baada ya majaribio matatu ya kutaka
kumuondoa madarakani kuambuliwa patupu.
Waandishi wanasema kuwa
serikali ililemazwa na vita villivyokuwa kati ya wafuasi wa Abdiweli
dhidi ya wale wanaoumuunga mkono rais Hassan Sheikh Mohamud.
No comments:
Post a Comment