maandamano
makubwa yametokea nchini Marekani katika mji wa St Louis
yaliyosababishwa na askari kumpiga risasi kijana mweusi akiwa katika
kituo cha mafuta .Polisi wanamtetea afisa mwenzao ya kwamba alitenda
kitendo hicho kama njia ya kujihami ,baada ya marehemu kumnyoonyeshea
bunduki katika kitongoji cha Berkeley.
Waandamanaji waliyaanza
maandamano hayo mara tu baada ya taarifa za mauaji hayo
kusambaa,kutokana na hasira waliyonayo waandamanaji hao picha za video
zinawaonesha baadhi yao wakivuka mpaka waliowekewa na polisi .
kitongoji
cha Berkeley kiko umbali wa kilomita tatu kutoka mjini Ferguson,
Missouri, mahali ambako yalifanyika mauaji ya kijana mwingine mweusi
aliyekuwa na umri wa miaka kumi na nane Michael Brown , aliyepigwa
risasi na askari wa kizungu,mauaji yaliyoibua hisia za ubaguzi wa rangi
,mauaji ambayo yalitokea mwezi August mwaka huu .hata hivyo Brown hakuwa
na silaha yoyote wakati akiauwa.
No comments:
Post a Comment