Uchunguzi
wa miezi mitatu uliofanywa na jarida la The Nairobian nchini Kenya
umebaini kwamba wakunga wa kiume huwadanganya wanawake wajawazito katika
makaazi ya mijini kufanya tendo la ngono kabla ya kujifungua.
Wao hufanya tendo hilo kwa madai ya kwamba litafungua njia ya mtoto ili kukwepa kufanyiwa upasuaji.
Afisa mmoja wa afya wilayani amesema kuwa udanganyifu huo huenda uko kila mahala.
Wanawake wengine wanadaiwa kukiri kulala na wakunga hao ili kukwepa kujifungua kupitia upasuaji.
Afisa
huyo ambaye jina lake tumelibana ameliambia The Nairobian kwamba visa
vya wakunga ambao hawakuhitimu wanaowadanganya wanawake sio vipya.
Anasema
kuwa katika warsha moja iliofanyika katika hospitali ya Pumwani jijini
Nairobi,baadhi ya wanawake walikiri kushikwa katika mtego huo.
Inadaiwa kuwa tatizo hilo limeenea hadi katika jamii kadhaa.
Hatahivyo afisa huyo amesema kuwa kitendo hicho kinahatarisha maisha ya mama anayetaka kujifungua.
Anasema kuwa ni uhalifu mkubwa kuwadanganya wanawake wajawazito.
Anasema
kwamba baadhi ya wanawake wamemfichua mwanamume mmoja katika mtaa wa
huruma jini Nairobi ambaye anadaiwa kulala na wanawake wajawazito kwa
kisingizio cha kutaka kufungua njia yao ya uzazi.
Anaongezea kuwa kitendo hicho humfanya mama mjamzito kuwa hatarini mwa maambukizi ya ukimwi na magonjwa mengine ya zinaa.
Mkunga mwandamizi katika hospitali ya Kenyatta ambaye alikataa kunukuliwa anasema kuwa visa vichache vimeripotiwa.
Afisa huyo ametoa wito kwa maafisa wa polisi kuwatumia wanawake wajawazito kuwakamata watu kama hao.
''Kufanya ngono kabla ya kujifungua sio suluhu iwapo kujifungua kwa mwanamke huyo kuna tatizo.''.
Ameongezea
kuwa,'' iwapo ni kweli kwamba ngono hufungua njia ya kizazi,basi ni kwa
nini wanawake hao wasilale na waume zao'',alihoji daktari huyo.
No comments:
Post a Comment