Costa akiifungia bao la pili Chelsea Uwanja wa Stamford Bridge
TIMU ya Chelsea leo imeshinda mechi ya tatu mfululizo ya Ligi Kuu ya England baada ya kuichapa West Ham United mabao 2-0 Uwanja wa Stamford Bridge, London.
Beki na Nahodha, John Terry aliifungia Chelsea bao la kwanza dakika ya 31 akimalizia kazi nzuri ya mshambuliaji Diego Costa.
Diego
Costa mwenyewe akafunga bao la pili dakika ya 62 akimalizia pasi ya
Eden Hazard, kabla ya kumpisha mkongwe Didier Drogba dakika ya 83.
No comments:
Post a Comment