JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
Hali ya
usalama barabarani kiujumla kwa mwaka huu 2014 ni ya kuridhisha ukilinganisha
na mwaka jana. Kwa mfano ukiangalia takwimu za ajali kwa miezi 11 ya mwaka
2013 Januari- Novemba kulinganisha na
takwimu ya ajali kwa miezi 11 ya mwaka 2014 Januari-Novemba utagundua kuwa kuwa
kuna upungufu wa ajali kwa asilimia 38.20 za ajali, asilimia 5.63 za vifo na
asilimia 28.27 za majeruhi.
|
Jan-Nov
2013
|
Jan-Nov
2014
|
Tofauti
|
Asilimia
(%)
|
Ajali
|
21,791
|
13,466
|
-8325
|
38.20
|
Vifo
|
3,642
|
3,437
|
-205
|
5.63
|
Majeruhi
|
18,813
|
13,495
|
-5318
|
28.27
|
Hata
hivyo, pamoja na juhudi hizi bado matukio ya ajali yanaendelea na tunashuhudia
yakichukua maisha ya ndugu na jamaa zetu huku yakiacha majeruhi, vilema na
uharibifu wa mali.
Ndugu
wanahabari,
Wito
wangu wa leo napenda kuwakumbusha Madereva na watumiaji wote wa barabara kuziheshimu
sheria na kanuni za usalama barabarani husasani katika kipindi hiki cha mwisho
wa mwaka kinachoambatana na sikukuu za Krismas na mwaka mpya.
Mtaungana
na mimi kwamba kumekuwa na ongezeko kubwa la ajali za barabarani miaka iliyopita
katika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka ambapo sababu kubwa za ongezeko hilo ni
za kibinadamu zikiwemo mwendo kasi, ulevi, matumizi ya simu za mkononi wakati
wa kuendesha, uendeshaji wa hatari (overtaking), kutofuata alama,michoro na
ishara za barabarani ,matumizi ya taa zenye mwanga mkali barabarani na
uegeshaji mbaya wa magari barabarani.
Ndugu
wanahabari,
Bado kuna
ukiukwaji wa sheria inayowataka wapanda pikipiki (madereva na abiria) kuvaa
kofia ngumu (helmet) muda wote wanapotumia vyombo hivyo. Tunawakumbusha
watumiaji wa vyombo hivyo kuzingatia matumizi ya kofia ngumu muda wote
wanapotumia vyombo hivyo hasa katika kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa
mwaka.
Ndugu
wanahabari,
Napenda
pia kuchukua nafasi kuwakumbusha askari wote kusimamia sheria na kanuni za
usalama barabarani kama wanavyoelekezwa, Kinyume na hapo hatua kali za kisheria
na kinidhamu zitachuliwa dhidi ya yeyote atakayekiuka. Niwaombe tu wananchi
mtoe ushirikiano kwa kutupatia taarifa za askari wanaokiuka taratibu zao za kazi
katika maeneo mbalimbali.
Ndugu
wanahabari,
Jeshi la
polisi Kikosi cha usalama barabarani limejipanga kikamilifu hususani
kimikakati kupambana na ajali za barabarani na kadhia zote za sikukuu za
mwisho wa mwaka kama nauli na ubabaishaji katika usafiri wa abiria. Tumekuwa na
kampeni zinazoendelea katika maeneo
mbalimbali nchini zinazolenga kutoa elimu ya usalama barabarani. Dhumuni kubwa
ni kupambana na makosa hatarishi yanayochangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la ajali
(mwendo kasi, ulevi, matumizi ya simu wakati wa kuendesha, kupita magari
mengine na uendeshaji wa hatari)
Katika
suala la nauli, tarehe 21/12/2014 kwa kutumia askari kanzu wa Jeshi la Polisi
tuliwakamata watu 7 waliokuwa wakiuza tiketi kwa bei kubwa katika kituo kikuu
cha Ubungo. Watuhumiwa hao tarehe 22/12/2014 walipelekwa mahakamani ambapo kesi
zao zitatajwa tena tarehe 5/1/2015 na 6/1/2015 na wako gereza la Segerea
wakisubiri tarehe hizo
1.Victor
Kombe –Wakala wa KVC
2.Mussa
Msangi- Karani wa tiketi HAPPY
NATION
3.Walter
Nkya - Karani wa tiketi IBRA LINE
4.Fredrick
Lema- Karani wa tiketi MBAZI TRAVEL
COACH
5.Ramadhani
Mbaga –Usafiri wa TOYOTA NOAH
6.Stephen
Amos – Usafiri wa TOYOTA NOAH
7.Jane
Gabriel - Usafiri wa TOYOTA NOAH
Aidha
jana tarehe 23/12/2014 asubuhi watu wengine 3 walikamatwa wakiuza tiketi kwa
bei ya juu ambao leo taratibu zikikamilika watapelekwa mahakamani,
1.Kassim
Azaria - Usafiri wa NOAH
2.Kelvin
Charles - Wakala wa Islam
3.
Mbaraka Tariba Kombo - Wakala wa Islam
Nipende
tu kuwajulisha watumiaji wote wa barabara kuwa
askari wataendelea kuwa wakali sana katika kipindi hiki ambapo hatua kali za kisheria zitachuliwa kwa
yeyote atakayekamatwa akivunja sheria za
usalama barabarani. Niwaombe tu watumiaji wote
wa barabara watii sheria bila shuruti .
Ndugu wanahabari,
Mwisho lakini sio kwa umuhimu napenda kuwaasa wananchi na wadau wa usalama barabarani kwa ujumla,
watupe ushirikiano zaidi kwa kutoa taarifa za uhalifu wa usalama barabarani,
kufuata sheria, kanuni na maelekezo kwa ajili ya usalama wao watumiapo barabara.
Kila mmoja atambue haki na wajibu wake akiwa barabarani ikiwa ni kuwa na subira
na kujali watumiaji wengine wa barabara kwani wana haki sawa ya kutumia
barabara. Watoto wasiachwe kutembea barabarani bila ya uangalizi wa watu
wazima.
Ninawatakia heri ya Xmas na Mwaka Mpya.
˝Maamuzi yako barabarani ni hatima
yetu-Fikiria kwanza”.
Imetolewa na:
MOHAMMED
R.MPINGA – DCP
KAMANDA WA POLISI,
KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI (T)
No comments:
Post a Comment