Wapiganaji wa Islamic State nchini Syria wamedai kuidungua ndege ya kivita ya muungano wa jeshi unaoongozwa na Marekani.
Shirika
linalochunguza maswala ya haki za kibinadamu lenye makao yake mjini
London ambalo linaunga mkono upinzani nchini Syria limesema kuwa ndege
hiyo ilianguka karibu na mji wa kazkazini wa Raqqa unaodhibitiwa na IS.
Shirika hilo linasema kuwa rubani, raia mwarabu aliyekuwa akiendesha ndege hiyo ametekwa.
Baadhi
ya ripoti zinadai kuwa rubani huyo ni raia wa Jordan.Jordan ni miongoni
mwa mataifa ya kiarabu ambayo yanashiriki katika mashambulzi dhidi ya
Islamic State.
No comments:
Post a Comment