Na Mwandishi Wetu
OFISA Utamaduni mkoa
wa Iringa, Mwesiga Muhambo amelikaribisha Tamasha la Krismasi mkoani
kwake kwa sababu ni siku ya kupokea zawadi duniani kote.
Kwa Mujibu wa Muhambo
badala ya kusubiri kupokea zawadi wajitokeze kwenye Tamasha la Krismasi
mkoani humo linalotarajia kufanyika Desemba 26 kwenye uwanja wa Samora.
“Zawadi yetu sisi
wakazi wa Iringa ni Tamasha la Krismasi ambalo tunapata neno la Mungu
kupitia waimbaji na viongozi mbalimbali wa dini,” alisema Muhambo.
Naye Kada wa Chama cha
Mapinduzi (CCM), Athumani Haule alitumia fursa hiyo kuikaribisha
Kampuni ya Msama Promotions mkoani humo kwa sababu ni fursa murua kwa
wakazi wa mkoa huo.
Haule alisema anaamini kupitia Msama zitapatikana fursa mbalimbali na kuongeza chachu katika nyanja mbalimbali.
Katibu Mkuu wa CCM Iringa, Hassan Mtenga alitoa wito kwa wakazi wa Iringa kujnitokeza kwa wingi katika tamasha hilo.
Mgeni rasmi katika tamasha hilo ni aliyekuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Fredrick Mwakalebela.
No comments:
Post a Comment