WAKATI Dunia ikisubiri saa kadhaa
kabla ya sherehe ya Sikukuu ya Krismasi, Wakazi wa mkoa wa Mbeya na
vitongoji vyake wamepewa wito na Umoja wa Kwaya ya makanisa mbalimbali
mkoani Mbeya kujitokeza kwa wingi kwenye Tamasha la Krismasi
linalofanyika (Desemba 25) leo kwenye uwanja wa Sokoine jijini humo.
Kwa Mujibu wa Mchungaji wa Kanisa la EAGT ambaye pia ni Mweka
hazina wa Kwaya hiyo, Zacharia Mwakasaka kwaya hiyo inatarajia
kushirikisha waimbaji zaidi ya 40 wa kwaya hiyo.
Mchungaji Mwakasaka alisema wanakwaya hao kwenye mkesha wa
sikukuu hiyo, Desemba 24 waliweka kambi ya siku moja kwenye chuo cha
Uyole kwa lengo la kujiweka sawa kabla ya Tamasha hilo.
Mwakasaka alitumia fursa hiyo kuwakaribisha wakazi wa Mbeya na
vitongoji vyake kujitokeza kwa wingi kushuhudia kwaya hiyo ambayo
imekusanya madhehebu mbalimbali ya Kipentekoste ya jijini humo.
Aidha Mwakasaka alisema Kwaya hiyo inatarajia kuzindua albamu
yake ya Mubhopege Pa Finganilo yenye nyimbo nane nyimbo nyingine ni kama
Ilisubha ‘Jua linachomoza’, Yesu alipokwenda, Jesu Bho Ikufyuka ‘Yesu
alipopaa’, Matendo, Gwe Kyala Mwikemo ‘Mungu Mtakatifu’ na Nasobhile
‘Nilikuwa nimepotea msituni’.
Mgeni rasmi mkoani Mbeya ni Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye.
No comments:
Post a Comment