Balozi Sefue
amemsimamisha kazi Ndugu Maswi kuanzia leo, Jumanne, Desemba 23, 2014,
kwa kutumia madaraka aliyonayo kama Mamlaka ya Nidhamu kwa Watumishi wa
Umma wanaoteuliwa na Rais, wakiwemo Makatibu Wakuu.
Taarifa iliyotolewa na
Ofisi ya Balozi Sefue mjini Dar es Salaam imesema kuwa amechukua hatua
hiyo “Kwa mujibu wa Kifungu 4(3) (d) cha Sheria ya Utumishi wa Umma, Na.
8 ya mwaka 2002 (kama ilivyorekebishwa)” ambapo “Katibu Mkuu Kiongozi
ndiye Mamlaka ya Nidhamu kwa Watumishi wa Umma wanaoteuliwa na Rais,
wakiwemo Makatibu Wakuu.”
Badala yake, Balozi
Sefue amesema kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini,
Mhandisi Ngosi C. Mwihava atakaimu nafasi ya Katibu Mkuu, Wizara ya
Nishati na Madini, hadi uchunguzi dhidi ya Ndugu Eliakim C. Maswi
utakapokamilika
No comments:
Post a Comment