Na: Goodluck Eliona na Mwinyi Sadallah, Mwananchi
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.
- Profesa Muhongo akataa kuzungumzia hatima yake
Vyama vya upinzani Zanzibar vimeshangaa kitendo
cha Rais Kikwete cha kutomwajibisha Waziri Mkuu Mizengo Pinda, wakati
huko nyuma kuna mawaziri akiwamo Waziri Mkuu waliwajibika kwa makosa
yaliyofanywa na watendaji wao.
Katibu Mkuu wa Chama cha Tadea, Juma Ali Khatibu
alisema kwamba kuna viongozi wengi ambao walilazimika kujiuzulu kwa
makosa ambayo hawakuhusika lili kulinda misingi ya uwajibikaji wa pamoja
na kushangaa serikali kuendelea kumlinda Waziri Mkuu Mizengo Pinda,
wakati kashfa hiyo imetia hasara taifa baada ya wahisani kusitisha
misaada yao.
Alisema kwamba kama Rais Kikwete ameamua kumuachia
Waziri Mkuu kuendelea na wadhifa wake wakati umefika kwa Serikali
kuwaomba radhi viongozi wote ambao walijiuzulu nyadhifa zao kwa makosa
ya wengine.
Upande wake Makamu Mwenyekiti wa Chadema Zanzibar,
Said Issa Mohamed alisema kwamba licha ya kuwa Waziri Mkuu Mizengo
Pinda, hakuhusika kuchota fedha hizo. lakini alitakiwa kujiuzulu ili
kulinda heshima yake na kupunguza hasira za wananchi.
“Kwa heshima ya misingi ya Utawala bora Kiongozi
hata kama hukuhusika moja kwa moja, unalazimika kuwajibika kulinda dhana
ya uwajibikaji wa pamoja.” alisema Mohamed.
Balozi Sefue asema Rais Kikwete ataamua hatima yake wakati wowote,
Upande wake Mkurugenzi wa Uenezi na Mawasiliano ya Umma wa CUF, Salim Bimani Abdalla alihoji ni kigezo gani kilichomfanya Mzee Ali Hassan Mwinyi akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Abdallah Said Natepe (marehemu), Shamsi Vuai Nahodha, Dk Emanuel Nchimbi na Balozi Khamis Kagasheki wajiuzulu lakini Pinda abaki katika Ofisi za umma.
Upande wake Mkurugenzi wa Uenezi na Mawasiliano ya Umma wa CUF, Salim Bimani Abdalla alihoji ni kigezo gani kilichomfanya Mzee Ali Hassan Mwinyi akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Abdallah Said Natepe (marehemu), Shamsi Vuai Nahodha, Dk Emanuel Nchimbi na Balozi Khamis Kagasheki wajiuzulu lakini Pinda abaki katika Ofisi za umma.
Mwinyi hakuwapo wakati mauaji yaliotokea mkoani
Shinyanga, Natepe hakujua kama kina Pius Lugangira, Hatibu Gandhi na
Christopher Kadego waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya uhaini kama
wangetoroka katika Gereza la Ukonga.
Nahodha, Dk Nchimbi na Balozi Kagasheki pia
hawakuhusika wala kufika katika eneo la utesaji wa watu wakati
utekelezaji wa Operesheni Tokomeza Ujangili.
Bimani alisema kwamba viongozi wote walioguswa na
kashfa ya escrow wanatakiwa kufukuzwa, kushtakiwa na mali zao
kutaifishwa na Serikali na kusisitiza kama serikali itashindwa kazi hiyo
itafanywa na Ukawa mara baada ya kuingia madarakani mwakani.
Makamu Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, Ambar Khamis
Haji alisema kwamba maamuzi ya Rais Kikwete yameshindwa kumaliza kiu ya
Watanzania wengi waliokuwa wakisubiri kuona viongozi waliohusika na
kashfa ya escrow wanafukuzwa na kufikishwa mahakamani na mali zao
kutaifishwa.
Alisema kinachoonekana sasa Serikali imeamua
kuwalinda wahalifu, kitendo ambacho hakitasadia kujenga misingi ya
utawala bora pamoja na kufanikisha vita dhidi ya rushwa na ufisadi.
Haji alisema kwamba ni jambo la kushangaza Rais
Kikwete amekuwa mzito kutekeleza uamuzi ya Bunge, wakati Serikali ni
sehemu ya bunge na ilishiriki katika kupitisha maazimio hayo baada ya
kamati za uchunguzi kuwasilishwa ripoti za uchunguzi.
No comments:
Post a Comment