Na Mwandishi Wetu
Mbunge wa Singida Kaskazini,
Lazaro Nyalandu, Desemba 28, 2014 (kesho J’pili) atafanya mkutano mkubwa
kwa ajili ya kumshukuru Mwenyezi Mungu na wananchi wa Singida Vijijini
na Watanzania wote kwa kutimiza miaka 15 ya ubunge.
Taarifa iliyotolewa na Katibu wa
Mbunge huyo, Elia Diga, imesema kuwa mkutano huo ambao utaambatana na
burudani mbalimbali, utafanyika katika Kata ya Ilongero na utahudhuriwa
na viongozi wa Chama na serikali, viongozi wa dini zote na wananchi
zaidi ya 20,000 kutoka kata zote zinazounda jimbo hilo na zile za
jirani.
Katika mkutano huo, Nyalandu
atahutubia wananchi pamoja na kueleza mafanikio ya utekelezaji wa Ilani
ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kipindi chote cha miaka 15.
Pamoja na mafanikio makubwa
yaliyopatikana mpaka sasa, Nyalandu pia ataeleza wananchi mwelekeo mpya
wa jimbo hilo na mahali anapopenda lifike.
Viongozi wote wa CCM Wilaya ya
Singida wakiongozwa na mwenyekiti wake, watahudhuria mkutano huo na
kutoa hotuba fupi kwa wananchi.
Wasanii nyota wanaotamba nchini
wakiongozwa na kundi la Makomandoo, Rose Muhando, Christina Shusho,
H-Baba, Mchekeshaji Steve Nyerere na Bendi ya New Life Bandi watakuwepo
kukonga nyoyo.
Pia kutakuwepo na vikundi
mbalimbali vya ngoma za asili vikiwemo Njagmba, Ilongero Group na
vingine vingi vitakuwepo kutoa burudani.
No comments:
Post a Comment