Mratibu wa Mpango wa Ujasiriamali
na Kukuza Ajira kwa Vijana ndani ya Shirika la kazi Duniani (ILO), Bw
Mkuku Luis akitoa hotuba yake wakati akifungua mafunzo ya ujarimali kwa
vijana yaliofanyika katika Desemba 19, 2014 jijini Dar es Salaam.
Afisa Habari wa Shirika la Umoja
wa Mataifa kitengo cha Mawasiliano (UNIC), Bi Usia Nkhoma Ledama
akielezea zaidi kuhusiana na mafuzo hayo kwa vijana
Vijana mbalimbali kutoka mkoa wa Dar es Salaam wilaya zote tatu za mkoa wakifuatilia mada mbalimbali wakati wa mafunzo hayo.
Mtoa mada Bw Ambokile Laurence akiwakilisha mada yake.
Mratibu wa Mpango wa Ujasiriamali na Kukuza Ajira kwa Vijana ndani ya Shirika la kazi Duniani (ILO), Bw Mkuku Luis.
…………………………………………………………..
SHIRIKA LA Kazi Duniani (ILO) kupitia mradi wake wa mafunzo ya
ujasirimali na kukuza ajira kwa vijana wameweza kutoa mafunzo
yaliyoanzisha takribani biashara 37,000 za vijana nchini nzima.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana
wakati ufunguzi wa mafunzo hayo ujasirimali kwa vijana, Mratibu wa
Mpango wa Ujasiriamali na Kukuza Ajira kwa Vijana ndani ya Shirika la
kazi Duniani (ILO), Bw Luis Mkuku amesema wana kuunga mkono juhudi za
vijana wakufunzi ya kukuza uelewa wa ujasirimali kwa vijana wenzao
nchini.
“leo tunatoa mafunzo ya ujasirimali kwa vijana kupitia wakufunzi
ambao ni vijana wenzao kuweza kuwafundisha na kuwatia moyo ili waweze
kujikwamua katika dimbwi la umaskini kwa kuanzisha biashara zao,”
aliongeza
Amesema vijana mara nyingi kukutana na watu ambao wanawakatisha
tamaa kuweza kufikia malengo na ndoto zao za kimaisha na mafunzo hayo
yanatolewa na ILO ili kuweza kumwezesha kijana kufikia malengo yake
maishani.
Mkuku alifafanua kwamba vijana wanaweza kuzikabili changamoto
zao kwenye maisha yao ya kila siku kwa kuweza kufikiria jambo mbadala
ikiwemo dhana ya kujitegemea kwa kuanzisha biashara zenye tija kwenye
maisha yao.
Amesema kwamba tangu mafunzo hayo yaanze kutolewa na shirika
hilo la kazi duniani ni miaka mitatu na wana wakufunzi wenye mbinu za
ujasiriamali nchi nzima na kwa mkoa wa Dar es Salaam wana wakufunzi
ishirini.
“vijana wengi wamekuwa na tatizo la kujiiingiza kwenye matumizi
ya dawa za kulevya kwa sababu wanakosa watu wa kuwashauri jinsi ngani ya
kuweza kujifunza stadi za maisha na kuanza maisha ya kujitegemea kwa
ufupi ni kwamba vijana wanaopotea kwenye madawa ya kulevya ni vipaji
vilivyopotea,” alisisitiza,
Kwa upande Afisa Habari wa Shirika la Umoja wa Mataifa kitengo
cha Mawasiliano (UNIC), Bi Usia Nkhoma Ledama amesema kwamba wameandaa
mafunzo kwa vijana wasiokuwa mashuleni na walioko kwenye biashara.
Alifafanua kwamba mafunzo haya yanawalenga vijana wote wasio
kuwa mashuleni na ambao waliokuwa katika matumizi ya madawa ya kulevya
ili waweze kukabiliana na changamoto za kila siku za maisha.
“mafunzo yanahusisha vijana wote wa mkoa wa Dar es Salaam kutoka
wilaya zote tatu za mkoa ni lengo la umoja wa mataifa kupambana na
tatizo la umaskini kama malengo ya milenia yanavyosema,” amesema
Bi Ledama aliongeza kwamba mafunzo hayo pia yanahusisha vijana
ambao pia wamo katika biashara lakini hapo mwanzo walifanya biashara
bila kuwa na ufahamu au uelewa wa kutosha kuhusu biashara.
Alifafanua kwamba mafunzo hayo yalianza miaka mitatu iliyopita
na inalenga kumtoa kijana katika hali ngumu ya maisha ikiwemo matumizi
ya madawa ya kulevya na kuweza kumwezesha kijana kujitegemea kwa
kuanzisha biashara ndogo ndogo.
No comments:
Post a Comment