JE, KWA HAYA BADO KUNA SERIKALI INAYOMILIKIWA NA WANANCHI,
ILIYOTOKANA NA WANANCHI, KWA AJILI YA KUTIMIZA MATAKWA YA WANANCHI
TANZANIA (DEMOCRACY)?.
(Ni ndefu lakini tumia muda wako kwa kutulia na kusoma)
Ndugu Watanzania wenzangu popote mlipo, nimshukuru mwenyezi Mungu
aliyetupa uhai mpaka muda huu tunasherekea sikukuu ya Noeli na namuomba
Mungu muweza atupe uhai tuuone mwaka mpya. Kwa wale waliotutoka kipindi
chote cha mwaka au siku za mwisho kuelekea kuumaliza mwaka, Mungu
aziweke roho zao mahala pema peponi. Amen...!
Nachukua fursa hii
adhimu ya kuelekea mwisho wa mwaka kuakisi tulikotoka, kuangalia tulipo
na kuchungulia (forecast) tuendako kama taifa la Tanzania na mustakbali
wa nchi yetu.
Ukweli ni kuwa niwe mimi, wewe na yule hakuna
sababu ya kunyamaza kama kuna jambo tunaweza kusema likaisaidia nchi kwa
ajili ya kizazi chetu na kijacho. Najua kuna watu (wepesi wa kukata
tamaa na kutotaka kuthubutu, wapendao business as ussual) wataniuliza
"wangapi wamepita wakashindwa kuibadilisha nchi hii, wewe ndo uweze?".
Ninachoamini ni kuwa wale wote wanaothubu kuongea kwa ajili ya ustawi wa
taifa letu kuna waliotangulia walipanda mbegu ya mawazo hayo ndani yao,
nao wasipofanikisha leo kuleta mabadiliko watoto wao wajukuu watayaleta
kwa sababu ya msingi wa mabadiliko unaojengwa leo. Vinginevyo watoto na
wajukuu wasingeyaleta kwa sababu wangeanza na msingi wenyewe.
Baada ya utangulizi huo bila kukuchosha, fuatana nami hatua kwa hatua kwa nilichokuandalia leo.
Kimsingi kukua au kutokua kwa nchi yoyote kiuchumi, kisiasa na kijamii
kunategemea dira, sera na usimamizi wa serikali husika iliyopo
madarakani.
Dira ni mwongozo wa taifa lolote ambayo kwayo, kila
serikali inayoingia madarakani lazima itengeneze sera zitakazosaidia
kufikia dira ya taifa. Dira ya taifa hulenga mipango ya muda mrefu kama
taifa (kama miaka 50 na zaidi) ambayo kwayo hujipambanua kwa mataifa
mengine. Mfano; enzi za Mwalimu, dira ya Tanzania ilikuwa ni kutengeneza
jamii yenye ujamaa na usawa inayojitegemea (kiuchumi na kijamii) ndiyo
maana katiba yetu ya 1977 ibara ya kwanza 3(1) inasema wazi kuwa
Tanzania ni nchi ya kijamaa, isiyofungamana na dini yoyote na inayofuata
demokrasia ya vyama vingi. Hili pekee linaipambanua Tanzania vilivyo.
Sera ni mipango ya serikali iliyopo madarakani (yenye dola) ambayo
kwayo serikali iliyopo madarakani inatekeleza mipango ya kutekeleza dira
ya taifa. Wakati wa Mwalimu alitengeneza sera ya vijij vya ujamaa ili
watu wakae pamoja, wakizalisha na kugawana walichozalisha kwa umoja.
Kwa sasa, kila mwenye akili za kawaida anatambua kuwa taifa letu
linaenda "bora liende" kama vile trekta lisilo na taa na dreva wake
analala usingizi wa pono kwenye usukani. Najua tuna watu wazuri ndani
yake ila "trekta” lilipopoteza mwelekeo linawapeleka msobemsobe.
Vyanzo vikuu vya hayo matatizo ni viwili.
1. Nchi kutokuwa na dira ya kufuata.
2. Kukosa viongozi wakuu bora ambao wapo tayari "ku-take risk" kwa lengo la "ku-reshape" nchi.
Wengi hawajui kuwa kama nchi sasa hatuna dira tunayofuata ili kuweka
wigo njia kwa kila mwananchi kwa kila anachokifanya kilenge kutufikisha
tunakotaka kama taifa. Tunajua sera ya Mwalimu ilikuwa ya ujamaa na
kujitegemea na aliibaini hivyo kwenye katiba. Sera hiyo iliposhindwa,
mambo yalianza kubadilika pole pole kuuelekea ubepari mpaka sasa ubepari
umekomaa labda muda si mrefu tutaingia ubeberu, lakini viongozi wetu
"kwa kumuogopa marehemu Mwali Nyerere" wameshindwa kuweka wazi kwenye
katiba kuwa nchi yetu inafuata misingi ya kibepari. Athari ya kutoliweka
wazi hili ni mvutano unaofanya tusinie mamoja kama taifa kuanzia kwa
wananchi mmoja mmoja mpaka viongozi wetu. Hivyo wakati wengine
wanapambana kuleta maendeleo kijamaa, wengine wanapambana kuleta
maendeleo kibepari hivyo ni mgongano mkubwa. Ukitaka kuamini kuhusu
hili, wafuate wabunge tofauti (rondom sampling) 5, waulize "Hivi
Tanzania tunafuata sera gani? Ya ujamaa au ubepari? Majibu usinipe kwa
sababu nayajua! Matokeo ya nchi kutokuwa na dira ya maendeleo ya nchi,
inaanza kuongozwa kwa sera tu (mipango ya aliyshika dola kwa kipindi
ambacho atakuwa madarakani). Akaja mtawala fulani akasema haoni umuhimu
wa masomo ya sayansi katika kuendeleza taifa hili na badala yale tuwe na
taifa la wacheza ngoma pekee, yanafutwa masomo ya sayansi na kubaki na
masomo ya kucheza ngoma pekee mashuleni ili kuzalisha wacheza ngoma tu.
Lakini nchi ingekuwa na dira, mfano: tunataka Tanzania iwe nchi ya
kijamaa inayoendeshwa na uchumi wa viwanda (msingi wa maendeleo duniani
kote) tungefanya "elimu hitajika" ndiyo nguzo pekee nchini. Siyo kilimo
ni uti w mgongo, siasa ni kilimo wala kilimo kwanza kwa sababu nchi
ikiwekeza katika elimu sahihi kwa watu wake ndipo maendeleo katika
nyanja zote yanawezekana. Kinachobakia baada tu ya kuwapa elimu, ni
kuwatengezea mazingira mazuri kila mwananchi mwenye ujuzi wa anachokijua
kukifanya "precisely". Tukajifunze kwa Rwanda ( mhh..! Najua watawala
hawaendi kuisikia kauli hii).
Shida kubwa ya pili tulionayo ni UONGOZI.
Taifa likifika lilipofikia hakuna tena kitakacholibadilisha mpaka mfumo
wa viongozi wote waliopo watoke, waingie wengine ambao watakuwa tayari
"ku-take highest risk ku-reshape" nchi. Si rahisi hata kidogo.
Umuhimu wa "ku-reshape" unatokana na;
1. Kukithiri kwa rushwa
1. Kukithiri kwa rushwa
Tumeshuhudi skendo za rushwa zinazovunja rekodi tangu nchi hii kupata.
Shida ni kuwa rushwa hiyo inapita mpaka kwa wanaotakiwa kukemea rushwa,
matokeo yake serikali nzima inamezwa mifukoni mwa mafisadi.
2. Kuzeeka kwa mawazo ya kiongozi.
Miaka 50 ni mingi sana kwa chaki kimoja kutawala nchi. Inafika wakati
hakuwi mawazo mapya ya kuiongoza nchi ilihal ili uongozi uwe bora mawazo
mapya na ubunifu vinahitajika. Kwa msingi huo, nawahakikishia Watanzani
kuwa tungeanza kuonana maendeleo Tanzania kama upinzani ungechukua nchi
2015 kisha 2020 tena ichukue Ccm na baadaye kila anayeharibu angejua
hachaguliwi tena. Matokeo yake ni maendeleo kwa wananchi.
3. Nepotism/ undugulism
Hili ni tatizo kubwa. Nenda kila sehemu, idara za serikali, vyombo vya
dola kwenye vyama vya siasa nk utakuta zile krimu zote ni za vigogo wa
serikali. Sisemi wao hawana uwezo na haki ya kufanya huko, laaah! Bali
fuatilia CV zao na fanya ulinganifu na kipindi cha Nyerere. Inamaana
nyerere watoto wake walikuwa mbumbumbu sana ukilinganisha leo ambapo
mfano; baba mNEC, mama mNEC, mtoto mNEC, mkwe mNEC, shemeji mNEC,
wakurugenzi wote BOT wenyewe, TISS wenyewe, nk.
4. Kushindwa kusimamia mipango yao na kila mtu kuwa na ya kwake serikalini.
4. Kushindwa kusimamia mipango yao na kila mtu kuwa na ya kwake serikalini.
Kuna suala la pembejeo na ununuzi wa mahindi napenda kulichukulia kama mfano wangu halisia wilayani kwetu Mbozi.
Kwanza serikali ilitangaza kununua mahindi wilayani Mbozi na kwingineko kwa kupima na kuyahifadhi ghalani huku ikizuia wafanyabiashara kupeleka mahindi nje ya nchi. Tangu serikali imepima mahindi hayo, wakulima/wafanyabiashara hawajalipwa pesa zao hadi leo. Kwa kweli watu sasa wanaamini shughuli ya kilimo ni biashara kichaa kwa sababu watu wapata mavuno na kupata neema ya soko zuri nje, mipaka huzuiwa kuwa serkali itayanunua na malipo yenyewe ndo huwa hivi. Mbons hatujasikia wafanyabiashara wa vinyago, nguo, cement nk wakipata soko zuri wakizuiliwa mipaka? Tunahisi kamfumo haka kamelenga kuwafanya wakulima watumwa wa kudumu kwa sababu hawana haki kabisa ya kupata bei nzuri ya mazao yao. Badala yake, mh. Godfrey Zambi aliwawezesha watu wake wa tatu wa karibu kisiasa ndiyo wakalipwa.
Kwanza serikali ilitangaza kununua mahindi wilayani Mbozi na kwingineko kwa kupima na kuyahifadhi ghalani huku ikizuia wafanyabiashara kupeleka mahindi nje ya nchi. Tangu serikali imepima mahindi hayo, wakulima/wafanyabiashara hawajalipwa pesa zao hadi leo. Kwa kweli watu sasa wanaamini shughuli ya kilimo ni biashara kichaa kwa sababu watu wapata mavuno na kupata neema ya soko zuri nje, mipaka huzuiwa kuwa serkali itayanunua na malipo yenyewe ndo huwa hivi. Mbons hatujasikia wafanyabiashara wa vinyago, nguo, cement nk wakipata soko zuri wakizuiliwa mipaka? Tunahisi kamfumo haka kamelenga kuwafanya wakulima watumwa wa kudumu kwa sababu hawana haki kabisa ya kupata bei nzuri ya mazao yao. Badala yake, mh. Godfrey Zambi aliwawezesha watu wake wa tatu wa karibu kisiasa ndiyo wakalipwa.
Zaidi ya hapo, naibu waziri
wa kilimo na ushirika akijibu swali la Mh David Silinde mbunge wa Momba
alimwambia mbolea ipo inakuja, lakini alipokuja mkurugenzi wa pembejeo
alisema hazitakuwepo. Kwa sababu hiyo, tutegemee balaa la njaa mwakani.
For all those, lazima tuunganishe nguvu zetu kulinusuru taifa letu kwa
kuiambia serikali ya CCM 2015 kapumzike uje tena kuomba 2020.
Nawatakia msimu mzuri wa sikukuu. Mungu awabariki.
No comments:
Post a Comment