Na. Mwandishi Wetu.
Tume ya Rais ya Uchunguzi wa
Operesheni Tokomeza itakusanya taarifa na kupokea malalamiko
yaliyotokana na utekelezaji wa Operesheni Tokomeza Ujangili Nchini mikoa
ya Mikoa ya Arusha, Manyara, Tabora, Singida na Dodoma.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa
tarehe 24 Desemba, 2014 na Katibu wa Tume hiyo, Bw.Frederick Manyanda,
Tume inatarajiwa kuendelea na zoezi la kukusanya maoni na taarifa
kuanzia tarehe 5 Januari , 2015 mpaka tarehe 21 Januari,2015 katika
maeneo mbalimbali ya kanda ya Kaskazini na Kati Nchini.
Katika kutekeleza jukumu hilo, Bw.
Manyanda ameeleza kuwa, Tume itatembelea Mkoa wa Tabora tarehe 4
Januari 2015 mpaka tarehe 8 Januari 2015 na itakuwa Mkoa wa Singida
tarehe 9 Januari,2015 mpaka tarehe 10 Januari,2015.
Aidha Tume itatembelea Mkoa wa Dodoma tarehe 11 Januari, 2015
mpaka tarehe 12 Januari 2015. Vilevile, Wakili Manyanda ameeleza kuwa
Tume itakusanya maoni Mkoa wa Manyara kuanzia tarehe 13 Januari, 2015
mpaka tarehe 16 Januari, 2015 na Tume itakuwa Mkoa wa Arusha tarehe 16
Januari 2015 mpaka tarehe 19 Januari,2015.
Mpaka sasa Tume ya Rais ya Operesheni Tokomeza imefanikiwa
kukusanya taarifa na kupokea malamiko yaliyotokana na utekelezaji wa
Operesheni Tokomeza katika mikoa kumi na tano (15) ya Tanzania Bara
ambayo ni Kigoma, Katavi, Rukwa, Mbeya Kagera, Geita, Shinyanga, Simiyu,
Mwanza Mara,Lindi,Mtwara,Ruvuma,Iringa, Morogoro.
Pamoja na mikutano hiyo, Bw.
Manyanda ametumia fursa hiyo kuwakumbusha na kuwaomba wananchi na
watanzania wa maeneo husika kuendelea kutuma taarifa na malalamiko
kuhusu utekelezaji wa Operesheni Tokomeza kwa njia ya barua, simu na
barua pepe ambapo ameeleza kuwa wananchi wanaweza kutuma barua kwa
Katibu wa Tume, Tume ya Uchunguzi wa Operesheni Tokomeza Ujangili, SLP
9050, Dar es Salaam na barua pepe kwenda
opereshenitokomeza@agctz.go.tz.Aidha, wananchi wa maeneo husika wanaweza
kutuma ujumbe mfupi wa maandishi kwa namba za simu za Tigo: 0714
826826; Vodacom: 0767 826826; Airtel: 0787 826826; na Zantel: 0773
826826.
No comments:
Post a Comment