TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, December 20, 2014

KAMANDA KOVA MGENI RASMI LEO KATIKA MCHEZO WA TASWA FC DHIDI YA MAKIPA WA LIGI KUU VODACOM TANZANIA


Kikosi cha Timu ya waandishi wa Habari nchini Tanzania(TASWA FC) leo kitashuka dimbani kukipiga dhidi ya timu ya kombaini ya Makipa wanaocheza ligi kuu ya Vodacom Tanzania, mchezo utakaopigwa kwenye Dimba la Uwanja wa Karume jijjini Dar es Salaam.

Akizungumzia mchezo huo mwenyekiti wa Taswa, Majuto Omary amesema kuwa mchezo huo ni wa kirafiki wenye lengo la kuweka Mahusiano mazuri baina ya waandishi na Makipa wanaocheza ligi kuu Ya Vodacom Tanzania.

"ni mchezo wa kirafiki ambao nadhani utakuwa ni kivutio kikubwa kutokana na Wachezaji wa TASWA FC kuwa katika hali ya kiwango cha juu kutosha kuwapima Wachezaji hao ambao muda mwingi utumia kuchezea nafasi ya Mlinda Mlango, hivyo kwao pia ni moja ya zoezi kutokana na kwamba watajitambua kuhusu Pumzi pamoja na kujenga Mahusiano Mema kati yao wenyewe, na kutokana na mchezo huo kuwa wa aina yake imetulazimu kumtafuta Mgeni Rasmi ili aje atazame mchezo huo kwani burudani ya leo ni kubwa, na mgeni wetu ni Kamanda Kova"amesema Majuto

Kikosi cha makipa kinatazamiwa kuomngozwa na Ivo Mapunda, Juma Kaseja, Dida, Ally Mstafa, Aishi Manula pamoja na wengine wengi huku kikosi cha Timu ya Waandishi wa Habari (TASWA FC) kinatazamiwa kuongozwa na Kocha Mchezaji Ally Mkongwe, Ibrahim Maestro Masoud, Juma Pinto, Sarehe Ally, Mwidini Sufiani, Mpalule Shaaban, Salum Jaba, na wengine Wengi.


MATATIZO YA NDOA NA UMRI

MWANAUME MKUBWA ANAYEOA MSICHANA MDOGO
Imekuwa ni kawaida katika jamii za kiafrika wanaume wenye umri mkubwa sana kuoa wasichana wenye umri mdogo ambao wanaweza hata kuwazaa.Katika hili imekuwa ni kama fashion kwa wasichana kiasi wamekosa hata zile haya walizokuwa nazo wazazi wetu enzi za zamani.

Wasichana wengi wametokea kujidumbukiza kuolewa na mababa wakubwa sana hari si kuwa wanapenda kuolewa na wazee waliowazidi umri kwa kiasi kikubwa.Wachache kati yao wanapenda kuolewa na watu wazima na wengi kati ya hao hawapendi kabisa ndoa za namna hiyo.

SABABU ZA MSINGI ZA KUFANYA WASICHANA WADOGO WALAZIMIKE KUOLEWA NA WANAUME WATU WAZIMA

Moja ya sababu ambazo inapeleka wasichana wadogo kukubali kuolewa na wanaume wakubwa waliowazidi umri sana ni Pesa,Sifa za majina ya wanaume jijini au nchi walizopo,Umasikini wa familia walizotoka.hapo zamani wanawake wengi waliolewa na wanaume kwa kukubali mapenzi ya dhati na kuzingatia maadili mazuri ya ndoa.hawakuangalia suala la pesa au kuolewa na watu wenye majina makubwamakubwa walipenda sana wanaume waaminifu na wachapa kazi, wao pesa ilikuwa ni majaaliwa ya Mungu.

Wasichana wa kileo wamekuwa na tamaa za harakaharaka kimasha na kutopenda kabisa kwenda kwenye ndoa yenye mashaka au dhiki za maisha.
Kila msichana amekuwa akimtamani mwanaume yeyote yule mwenye pesa ili mradi akafaidi maisha ya kileo na uhakika wa kila anachokiona kipya akipate.

Mabinti wa kisasa hawapendi kujituma kama wale wa zamani ambao walikuwa wakitwanga,wakichota maji,wakifua na hata kulima na kusaidia mifugo pamoja na waume zao,siku hizi mtoto wa kike unamkuta hataki kucha zake zikatike kwa kufua au kumsaidia mumewe kufua.

Wengi wa wasichana wamekuwa na kasumba ya kuolewa na mwanaume yoyote yule mwenye pesa ili kuondokana na umasikini wa familia zao bila kufanya uchunguzi wowote ambao uleta hathari katika ndoa zao.

MATATIZO YA NDOA NA UMRI (ATHARI)
Uchunguzi nilioufanya katika wana ndoa wengi toka jamii za kiafrika wanapatwa na matatizo mengi ndani ya ndoa zao muda mchache tu mara ya kuingia katika ndoa na watu wasiowafanyia uchunguzi wa kina kabla ya kukubali kuolewa.

Tukianzia kwa upande wa wasichana ambao wamekuwa wakuimizwa sana na wanaume waliokubali kuolewa nao kwa kufuata pesa ili kujikomboa kutoka hari fulani ya kiwango cha chini kimaisha na kwenda huko kwa matajiri wakifikiri watapata ahueni kwao.Au  wale waliopenda kuolewa kwa kufuata umaarufu wa wanaume wenye majina makubwa(Famours People).

Wanaume wengi wanawalaghai wasichana wadogo kwa ahadi bandia [fake] pindi wanapotaka kuwa nao,wengine uwapa magari kama zuga toto ili wakubali kuolewa nao,wengine uwadanganya kwa kuwajengea nyumba.

(Athari namba Moja)

Wengi wa wasichana wamezikwa kwa ukimwi kutokana na tamaa za kuolewa na wanaume wakubwa hari ya kutaka maisha mazuri kwa kuona nikiolewa na mwenye pesa nitaneemeka kimaisha.

(Athari namba mbili)

Wengine wameathirika kisaikolojia kwa kulazimika kukubali kuwa wake wenza hari ya kuwa hawakutarajia haya mwanzoni.

(Athari namba Tatu)
Kadhalika wasichana wengi wamekuwa wakiteseka na ndoa zao kwa kutopata mapenzi waliyotarajia na hii inatokana na wanaume wengi wenye pesa kukosa muda wa kukaa na wake zao kutokana na shughuli za kazi zao zinavyowabana.

(Athari namba Nne)
Wengi wa wanaume wenye pesa ni wahuni kiasi kwamba wanawatesa wasichana wengi waliojiingiza bila kufanya uchunguzi wa kina kabla ya kuolewa nao.Na matokeo yake wanabaki na simanzi kila kukicha kwa kushindwa kuondoka kwenye ndoa wakifikiri watachekwa na wenzao au jamii inayomzunguka kutokana na sifa walizozifuata wakizani watazikosa maishani…
Kwa leo tuishia hapa mpaka juma lijalo

Na

Mwandishi wako Maganga One
magangaone@gmail.com

Rais Kikwete atunuku kamisheni kwa maafisa wapya wa jeshi


D92A3114Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpa zawadi na kumpongeza Luteni Usu Edwin Engelbert Kessy wakati wa hafla ya kutunuku kamisheni maafisa wa jeshi baada kuibuka mwanafunzi bora wakati wa mafunzo ya maafisa wa jeshi yaliyofanyika katika chuo cha jeshi Monduli mjini Arusha D92A3118Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Luteni Usu Edwin Engelbert Kessy wakati wa hafla ya kutunuku kamisheni maafisa wa jeshi baada kuibuka mwanafunzi bora wakati wa mafunzo ya maafisa wa jeshi yaliyofanyika katika chuo cha jeshi Monduli mjini Arusha D92A3178Rais Kikwete akitunuku Kamisheni maafisa wa jeshi katika chuo cha Jeshi huko Monduli Mkoani Arusha leo.Jumla ya maafisa 171 walitunukiwa kamisheni wakati wa hafla hiyo.
(picha na Freddy Maro).

 Rais Jakaya Kikwete akizungumza na Waziri Mkuu wa Mstaafu Mhe  Edward Lowassa walipohudhuria sherehe za kutunukiwa kamisheni maofisa wapya wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa cheo cha Luteni Usu, iliyofanyika katika chuo cha jeshi hilo Monduli, mkoani Arusha 
 
Picha ya pamoja
 Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Mhe.  Edward Lowassa akiongea na  maofisa waandamizi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania akiwemo na Mkuu wa Majeshi, Davis Mwamunyange (kushoto) kwenye sherehe za kutunukiwa kamisheni maofisa wapya wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa cheo cha Luteni Usu, iliyofanyika katika chuo cha jeshi hilo Monduli, mkoani Arusha.
 Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange akimkaribisha Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Mhe. Edward Lowassa alipowasili kwenye sherehe za kutunukiwa kamisheni maofisa wapya wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa cheo cha Luteni Usu, iliyofanyika katika chuo cha jeshi hilo Monduli.
 Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Mhe. Edward Lowassa (kulia) akizungumza na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi walipohudhuria sherehe za kutunukiwa kamisheni maofisa wapya wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa cheo cha Luteni Usu, iliyofanyika katika chuo cha jeshi hilo Monduli.
 Maofisa wapya wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa cheo cha Luteni Usu wakila kiapo cha utii mbele ya Rais Jakaya Kikwete baada ya kutunukiwa kamisheni katika chuo cha jeshi hilo Monduli, mkoani Arusha.
  Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange akiongea na Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Mhe. Edward Lowassa kwenye sherehe hizo.
 Burudani katika sherehe hizo
 Maofisa wapya wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa cheo cha Luteni Usu wakitembea kwa ukakamavu walipokuwa wakitoa heshima kwa Rais Jakaya Kikwete katika sherehe za kutunukiwa kamisheni maofisa hao, Monduli, mkoani Arusha
  Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange akiongea na Waziri  Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Mhe. Edward Lowassa. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.Daudi Felix Ntibenda
Wimbo wa Taifa ulipopigwa

WAIMBAJI WA TAMASHA LA KRISMAS MKOANI MBEYA WAELEZEA MAANDALIZI YAO

1Mwimbaji wa muziki wa injili Tumaini Njole akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za kampuni ya Msama Promotion ambayo inaandaa Tamasha la Pasaka litakalofanyika sikukuu ya Krismas tarehe 25/12/2014  mkoani Mbeya wakati alipozungumzia maadalizi ya tamasha hilo na jinsi alivyojipanga kukonga mioyo ya mashabiki wa nyimbo za injili mkoani Mbeya , Tamasha hilo linatarajiwa kuanza muda wa Saa nane mchana viingilio vikiwa ni shilingi 5000 kwa watu wazima na watoto shilingi 2000, Katika tamasha hilo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu Mstaafu Mh. Fredrick Sumaye na waimbaji wengine watakaotumbuiza ni Faraja Ntaboba, Upendo Nkone, Upendo Kirahilo, Rose Muhando, Bony Mwaiteje Edson Mwasabwite, Ambwene Mwasongwe na wengine wengi, Pia matamasha mengine yanatarajiwa kufanyika mkoani Iringa tarehe 26/12/2014 na Songea tarehe 28/12/2014, Katika Picha kushoto ni Mwimbaji Joshua Mlelwa. 2Mwimbaji wa muziki wa Injili Edson Mwasabwite akifafanua jambo wakati wa mkutano huo uliofanyika leo jijini Dar es salaam , Kushoto ni mwimbaji Joshua Mlelwa na katikati ni Mwimbaji Tumaini Njole 3Mwimbaji Joshua Mlelwa akielezea maandalizi yake wakati wa Tamasha la Pasaka litakalofanyika mkoani Mbeya wakati wa Sikukuu ya Krismas kulia ni Mwimbaji Tumaini Njole.

HUJUMA YA RAIS KIKWETE YAFICHUKA,DK SLAA ANASA UJUMBE KATI YA JK NA RUGIMALIRA SOMA HAPA KUJUA


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimedai kimenasa ujumbe mwingine wa barua pepe ulioandikwa na mmiliki wa Kampuni ya VIP Engeering, James Rugemalira, kwenda kwa Rais Jakaya Kikwete ukimtaka asitekeleze maazimio yaliyofikiwa na Bunge kuhusu akaunti ya Tegeta Escrow, mpaka uamuzi wa mahakama utakapotolewa.

Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Wilbroad Slaa, aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Alisema barua pepe hiyo iliyoandikwa Desemba mosi, ni mfululizo wa zile alizoandika Novemba 29, mwaka huu, zinazoanza kwa kumtaja ‘Dear JK’  kumweleza kuwa, ameshangazwa na maamuzi ya Bunge na maswali 21 kuhoji mhimili huo.
Alisema siku hiyo ya Novemba 29, alimwandikia kuomba amsaidie kuharakisha mradi wake wa hospitali anaotarajia kuijenga Bukoba.

Kwa mujibu wa Dk. Slaa, barua pepe ambazo zimekuwa zikiandikwa na Rugemalira ni kithibitisho tosha kwa kile kinachocheleweshwa maazimio yaliyofikiwa na Bunge.
“Sakata la Escrow bado ni bichi sana limeleta mgongano wa mihimili miwili, hii ni dira sahihi nchi haina maamuzi, tumeshtushwa Kikwete anamtii mtu binafsi badala ya Bunge,” alisema.

Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho bara, John Mnyika, alisema mashauri yaliyofunguliwa mahakamani, tayari Chadema imemtuma Wakili wa utetezi, Peter Kibatara, kufahamu msingi wa kesi ni upi.
Mnyika alisema baada ya chama kujiridhisha kuhusiana na msingi wa kufunguliwa mashauri hayo, sekretarieti ya chama itayajadili na kuyatolea maamuzi baadaye.

Aidha, alitoa wito kwa Rais Jakaya Kikwete kutoa mwelekeo na msimamo wake kuhusu maazimio ya Bunge yaliyofikiwa kwa sababu hakuna hukumu yoyote ya kuyafuta iliyotolewa na mahakama.
“Wamesema Kikwete atazungumza na wazee lakini wameahirisha hadi Jumatatu, hata kama yupo Arusha kule kuna wazee anaweza kuzungumza sehemu yoyote ikiwa yupo nchini, aliahidi atalitolea maamuzi suala hilo wiki moja sasa ni wiki ya pili,” alisema.

Kuhusu kauli ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi, Profesa Anna Tibaijuka kuwa, akijiuzulu Rais atashangaa, Mnyika alisema Kikwete anatakiwa kueleza kama anakubaliana na hilo.
“Nina taarifa za ndani ya Ikulu kuwa, inataka kufanya uchunguzi wake, Takukuru wameshakabidhi ripoti ya pili ya nyongeza, kwa hiyo ipo sababu ya Rais kuchukua hatua, endapo hatua hazitachukuliwa tutaeleza hatua gani tutachukua,” alisema.

UCHAGUZI S/MITAA
Dk. Slaa alisema Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Hawa Ghasia wajiuzulu, kwa kusababisha uchaguzi wa serikali za mitaa kuvurugika.
Alisema licha ya wananchi kupiga kura, baadhi ya maeneo wasimamizi wa uchaguzi kwa makusudi wamegoma kutangaza matokeo na wengine wameuvuruga kwa sababu CCM imeshindwa.
Alisema wana taarifa za kubadilishwa majina ya walioshinda Ngara na Igunga.

Pia alisema ipo nyaraka ambayo mkurugenzi anamwagiza mtendaji ahakikishe CCM kinashinda.
Aidha, alisema suala la kupita bila kupingwa ni kinyume na demokrasia na haki ya msingi ya raia ya kuchagua na kupendekeza kutumike kura za ndiyo au hapana.
Kadhalika Kamati kuu ya chama hicho imezitaka mamlaka zinazohusika kuwatambua mabalozi wa Chadema katika masuala yote yanayohitaji watu wa ngazi hiyo ikiwemo utambulisho wa ukazi.

UCHAGUZI MKUU

Alisema Kamati Kuu imepokea kwa masikitiko taarifa zinazoonyesha kuwa, hadi sasa serikali kupitia Tume ya Taifa ya Uchaguzi haionekani kujipanga kufanikisha uchaguzi huo.
Alisema juzi alitembelea vituo vya jimbo la Kawe na kubaini mashine ambazo serikali ilisema kuwa ni za kisasa,  ni mbovu na tayari amewasiliana na tume.
Mkurugenzi wa Usalama Chadema, John Mrema alisema Chadema imepeleka hati ya dharura namba 2 Mahakama ya Kinondoni kupinga mshindi wa mtaa wa Kiluvya kata ya Goba, asiapishwe na mahakama itamke kuwa uchaguzi wa nafasi ya Mwenyekiti na wajumbe viti maalum ni batili

DR. SHEIN AHUDHURIA MAHAFALI YA 10 YA CHUO KIKUU CHA TAIFA SUZA ZANZIBAR.

unnamedRais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae pia Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Zanzibar (Suza) Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Makamu Mkuu wa Chuo Prof Idriss Ahmada Rai mara baada ya kuwasili  katika ya Kampasi ya Chuo Tunguu kufungua Mahfali ya 10 yaliyofanyika chuoni hapo leo Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.[Picha na Ikulu.] unnamed1 Baadhi ya wanafunzi waliohitimu  mafunzo yao katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) wakiwa katika maandamano  katika mahfali ya 10 ya Chuo hicho yaliyofanyika leo kampasi ya Tunguu Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.[Picha na Ikulu.] unnamed2 Baadhi ya walimu katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) wakiwa katika maandamano  katika mahfali ya 10 ya Chuo hicho yaliyofanyika leo kampasi ya Tunguu Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae pia Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Zanzibar (Suza) Dk.Ali Mohamed Shein.[Picha na Ikulu.] unnamed3Wajumbe wa Baraza la Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) wakiwa katika maandamano yaliyoandaliwa rasmi katika mahfali ya 10 ya Chuo hicho katika kampasi ya Tunguu Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja leo ambapo mgeni rasmi akiwa .Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae pia Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Zanzibar (Suza) Dk.Ali Mohamed Shein[Picha na Ikulu.] unnamed4Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) Said Bakari Jecha (kushtoto) akifuatana na Viongozi akiwemo Mkuu wa Chuo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) wakati wa maandamano katika mahfali ya 10 ya Chuo Hicho yaliyofanyika leo katika Kampasi ya Tunguu Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.[Picha na Ikulu.] unnamed5 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae pia Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Zanzibar (Suza) Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipoku wa akiteta na Makamu Mkuu wa Chuo Prof Idriss Ahmada Rai wakati wa maandamano katika mahfali ya 10 ya Chuo Hicho yaliyofanyika leo katika Kampasi ya Tunguu Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.[Picha na Ikulu.] unnamed7 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae pia Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Zanzibar (Suza) Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) Makamu Mkuu wa Chuo Prof Idriss Ahmada Rai,Waziri wa Elimu na mafunzo ya Amali Ali Juma Shamuhuna na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Dk.Idriss Muslim Hija  wakisimama  wakati Wimbo wa Taifa Ukipigwa  katika mahfali ya 10 ya Chuo  yaliyofanyika leo katika Kampasi ya Tunguu Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.[Picha na Ikulu.] unnamed8Wazazi  na Watoto wa ambao wamefika katika viwanja vya mahfali ya 10 ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) wakishuhudia wahitimu wanapotunukiwa Vyeti,Stashahada na Shahada na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) leo ambae ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) .[Picha na Ikulu.] unnamed9 Baadhi ya wahitimu katika Mahfali ya 10 ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) waliotunukiwa  Stashahada ya Sayansi ya Kompyuta wakiwa katika viwanja vya Mahfali hayo katika kampasi ya Chuo Tunguu Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja   mgeni rasmi akiwa  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein ambae pia Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) .[Picha na Ikulu.] unnamed10Viongozi waliohudhuria katika Mahafali ya 10 ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) yaliyofanyika leo katika Kampasi ya Chuo Tunguu Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja (kutoka kushoto) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dk.Mwinyihaji Makame Mwadini,Katibu Mkuu Kiongozi Dk.Abdulhamid Yahya Mzee na Mkuu wa  Mkoa wa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis,[Picha na Ikulu} unnamed11 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein ambae pia Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Zanzibar (SUZA)alipokuwa akiwatunuku Vyeti,Stashahada na  Shahada  kwa wahitimu wa fani mbali mbali katika Mahfali ya 10 ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) yaliyofanyika leo katika Kampasi ya Chuo Tunguu Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja (kushoto) Makamu Mkuu wa chuo Prof Idriss Ahamada Rai,[Picha na Ikulu.]
unnamed
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein ambae ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) akimkabidhi zawadi Hamad Abdalla Nassor akiwa ni miongoni mwa wanafunzi bora waliofanya vizuri zaidi katika masomo yao wakati wa mahfali ya 10 ya Chuo hicho yaliyofanyika leo katika kampasi ya Chuo Tunguu Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja,[Picha na Ikulu.]
unnamed2
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein ambae ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) akitoa hutuba yake katika mahfali ya 10 ya chuo hicho yaliyofanyika leo katika kampasi ya Chuo Tunguu Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja,[Picha na Ikulu.]

Kuahirishwa kwa sherehe za SHIWATA

indexNa Mwandishi Wetu

SHEREHE za miaka kumi ya kuanzishwa kwa Mtandao wa WAsanii Tanzania (SHIWATA)zilizokuwa zifanyike Desemba 25, jijini Dar es Salaam zimeahirishwa.
Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Taalib alisema jana kuwa kuahirishwa kwa sherehe hizo kumetokana na wanachama wengi ambao walitakiwa kukabidhiwa nyumba zao kuwa katika sherehe za Krismas nje ya mkoa wa Dar es Salaam.
Alisema kuahirishwa huko kumesababisha pambano la watani wa jadi la Simba na Yanga Veterani lililokuwa lichezwe Desemba 25 kwenye uwanja wa Azam, Charambe mpaka litakapotangazwa tena. Mwenyekiti Taalib alisema sababu nyingine ya kuahirishwa kwa sherehe hizo ni kutokana na maombi ya mgeni rasmi ambaye hakumtaja kuwa yuko nje ya nchi kikazi ambaye aliomba ahudhurie tamasha hilo la kihistoria. Nyumba ambazo zitakabidhiwa ni 38 ambazo zimejengwa na kukamilika ambako wanachama hao walichangia ujenzi kwa kutoa fedha kidogo kidogo kupitia benki na kuchangua aina ya nyumba anayoitaka kutokana na kiasi alizochangia. Ili kuwapatia makazi ya bei nadfuu wanachama wake SHIWATA inajenga nyumba za sh. 631,000, sh. 1,500,000, sh. 3,800,000 na sh. 6,400,000 ambazo mwanachama anagaiwa kila mwezi Juni na Desemba kila mwaka..
Alisema katika makabidhiano hayo wamiliki wa nyumba hizo pia watakabidhiwa vyeti maalum vya kumaliki nyumba zao katika sherehe kubwa itakayofanyika kijiji cha Mwanzega, Mkuranga. Mpaka sasa SHIWATA ina wanachama 8,000.

SAKATA LA ESCROW LIMECHANGIA KUPUNGUZA KURA ZA CCM MKOANI IRINGA

Katibu wa chama cha mapinduzi mkoani Iringa HASSAN MTENGA akiongoza makatibu wa wilaya kuongea na waandishi wa habari mkoani Iringa
………………………………………………………………………………………..
Na Fredy Mgunda,Iringa
Katibu wa chama cha mapinduzi CCM HASSAN MTENGA amekiri kuhusu sakata la fedha za tegeta ESRWO na IPTL kuwa limechangia kudondoka katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika hivi karibuni. Akizungumza na waandishi wa habari amesema kuwa suala hilo lilihitaji elimu kubwa kuwaelimisha wananchi kabla ya uchaguzi huo wa serikali za mitaa.
Mtenga amesema dalili za awali kuhusu uchaguzi mkuu utakao fanyika mwakani ni nzuri kuhusu chama cha Mapinduzi na watashinda kwa kishindi kama uchaguzi wa serikali za mitaa. Aidha amezungumzia kuhusu vijana walioondoka katika chama cha mapinduzi na kujiunga na Chadema kuwa umetumika ujanja wa kuwa nunua vijana ili kupigia kura chama cha demokrasia na maendeleo Chadema. Kwa upande wa chama cha mapinduzi wilayani mufindi mkoani Iringa wameulalamikia uongozi wa serikali uliopewa dhamana ya kusimamia zoezi zima la uchaguzi wa serikali za mitaa ambapo dosari nyingi zimejitokeza tofauti na chaguzi zilizopita. Akizungunza na na mtandao huu katibu wa chama hicho wilayani mufindi MIRAJI MTATARU amesema kuwa uchaguzi huu umekuwa na changamoto nyingi hivyo kupelekea ucheleshaji wa vifaa pamoja na kufanya uchaguzi kuwa kama wa kushitukiza wakati walikuwa wamejipanga kwa muda muda mrefu. MTATURU ameitaka serikali iangalie kwa makini suala hili la uchaguzi kwa kuwa kuna wananchi wengi wamekosa haki yao ya msingi kwa kuwa walishindwa kupiga kuwa kutokana na kukosekana kwa karatasi za kupigia kura.
Aidha MTATURU amewapongeza wananchi wa wilaya ya mufindi kuendelea kukipigia kura wagombea wa CCM na kuwapa ushindi wa asilimia 99 na kuwaachia wapinzania asilimia moja tu licha ya changamoto zilizojitokeza kwenye uchaguzi huo.

Mwanahabari Kibiki atangaza kuwania Ubunge jimbo la Iringa mjini

Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa Frank Kibiki aliyetangaza nia
Na Fredy Mgunda,Iringa
………………………………………………………………………………
MJUMBE wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa, Frank Kibiki, ametangaza nia ya kuwania ubunge wa jimbo la Iringa mjini, kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).Akizungumza na waandishi wa Habari leo ofisini kwake, Kibiki amesema ni wakati wa vijana kushika hatamu kwa kuwania nafasi mbali mbali, ndani ya CCM na hatimaye kwenye umma wa watanzania.Kibiki ambaye ni Katibu mwandamizi wa Umoja wa Vijana, katika wilaya mbali mbali nchini amesema ameamua kuomba kupitishwa nafasi hiyo na CCM ili aweze kusaidiana na wananchi wa manipaa ya Iringa katika kuwaletea maendeleo.
Mjumbe huyo wa Mkutano mkuu wa CCM Taifa, amedai kuwa zipo changamoto nyingi zinazowakabili vijana na wananchi kwa ujumla na kwamba, njia pekee ya kuzitatua ni kuwa na uwakilishi toka miongoni mwao kwenye vyombo vya maamuzi. Kitaaluma, Kibiki ni mwandishi wa habari mwandamizi kupitia magazeti ya Uhuru na Mzalendo, mkoani Iringa.

Waimbaji wafanikiwa na semina Basata

index
Na Mwandishi Wetu

WAKATI  Tamasha la Krismasi liko mbioni kufanyika katika mikoa ya Mbeya, Iringa na Ruvuma wilaya ya Songea, Kampuni ya Msama Promotions inayoandaa tamasha hilo imeeleza kwamba waimbaji wengi walioshiriki semina zinazondaliwa na kampuni hiyo kwa kushirikiana Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) wamefanikiwa. Kampuni ya Msama Promotions huandaa semina hizo kwa sababu ya kuwaweka sawa waimbaji kabla ya kupanda jukwaani yakiwemo maadili. Kwa mujibu wa Katibu wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Jimmy Rwehumbiza mbali ya kuwa kuna changamoto ya waimbaji kutohudhuria katika semina hizo, ambao wanahudhuria wanafaidi mbinu mbalimbali pamoja na kujua haki zao. Alisema  katika semina hiyo waimbaji wanajifunza mambo mbalimbali ikiwemo mikataba. Rwehumbiza alisema kuwa faida nyingi zimepatikana kupitia semina hizo ambazo zimefanyika kwa muda mfupi ambako waimbaji imewasaidia kujisajili katika Baraza hilo na kutambulika kisheria ili kuwarahisishia mambo mbalimbali yakiwemo safari za nje ya nchi. Mwimbaji wa nyimbo za Injili, Edson Mwasabwite alisema kilio chao kikubwa ni kuibiwa kwa kazi zao huku akiilalamikia  Serikali kuwa imewatupa bila kuwasaidia katika kutatua tatizo hilo la wizi unaozidi kila kukicha. Mwimbaji huyo pia aliishukuru kampuni ya Msama Promotions ambayo imekuwa ikifanya kazi kubwa ya kukamata wazalishaji wa kazi feki za wasanii hapa nchini. Basata kupitia Ofisa wake Kwirujira Ng’oko Maregesi, aliwataka waimbaji hao kupitia Chama chao kumtumia mwanasheria wao na kusisitiza waimbaji kusimamia kazi zao na kutambua mikataba yao. Mbali na hayo pia Basata iliwaasa waimbaji kuacha kuuza kazi zao halisi ‘Master’ kwani kufanya hivyo ni kuwatajirisha wanaowauzia wasambazaji, ambako aliwataka waimbaji kuimba kwa kutumia vyombo kwani Watanzania wamechoka na mfumo wa ‘Play back’. Naye mdau aliyepata fursa ya kushiriki semina hiyo John Melele alisema serikali ilaumiwe kwa kushindwa kudhibiti tatizo hilo huku akitoa ushauri kiundwe chombo kitakachoifikia kila Halmashauri ya Mkoa na kuwatumia watendaji watakaoshughulikia masuala hayo huku akisisitiza kuwa kuwaachia waimbaji na msambazaji.

Kwaya maalum Mbeya yatinga kambini kuibeba Krismasi

imagesNa Mwandishi Wetu

KWAYA maalum jijini Mbeya wiki iliyopita iliingia kambini kwa siku moja kujiandaa na uzinduzi wa albamu yao ya Mubhopeghe Pa Finganilo (Kimbilieni kwenye ahadi) yenye nyimbo nane.
Kwa mujibu wa Mchungaji wa Kanisa wa EAGT, Zacharia Mwakasaka kambi hiyo inashirikisha waimbaji ambao ni Maaskofu, Wachungaji na viongozi mbalimbali wa dini waliomo kwenye Kwaya hiyo.
Mwakasaka alisema uzinduzi huo unashirikisha waimbaji, maaskofu na wachungaji waliopita kwenye mikono ya mzee Amulike Mwakiteka (84).
Mwakasaka alisema kupitia uzinduzi huo waumini mbalimbali watajionea viongozi hao ambao wanaongoza makanisa mbalimbali hapa nchini.
Mwakasaka alizitaja nyimbo zilizoko kwenye albamu hiyo ni pamoja na Mubhopeghe Pa Finganilo, Lazaro, Ilisubha ‘Jua Linachomoza’, Yesu alipokwenda, Jesu Bho Ikufyuka ‘Yesu alipopaa’, Matendo, Gwe Kyala Mwikemo ‘Mungu Mtakatifu’ na Nasobhile ‘Nilikuwa nimepotea Msituni’

Mwakalebela mgeni rasmi Tamasha la Krismasi Iringa

index
Na Mwandishi Wetu

ALIYEKUWA Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Fredrick Mwakalebela Desemba 26 anatarajia kuwa mgeni rasmi kwenye Tamasha la Krismasi mkoani Iringa.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama Mwakalebela anatarajia pia kuwaongoza waumini mbalimbali mkoani humo kwa lengo la kumtukuza Mungu kupitia waimbaji mbalimbali hapa nchini.
Msama alisema Mwakalebela atafanikisha lengo la kusaidia wenye uhitaji maalum kama Yatima, Wajane na walemavu ambao wanahitaji msaada mkubwa kutoka kwa wadau mbalimbali.
Msama alisema Mwakalebela ni mdau ambaye anatakiwa aendane na kauli mbiu ya Tanzania ni yetu, Tuilinde na Kuipenda ambayo inachochea wadau ambao wanatakiwa kusaidia wadau hao.
Tamasha hilo linatarajia kuanza Desemba 25, kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya kabla ya kuhamia Iringa  na kumalizia Desemba 28 Wilayani Songea kwenye uwanja wa Majimaji.

HABARI MBALIMBALI KUTOKA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TFF

index
Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana jana (Desemba 19 mwaka huu) jijini Dar es Salaam, imezingatia upungufu uliopo katika utekelezaji wa matumizi ya tiketi za elektroniki.
Hivyo, Kamati hiyo imeiagiza Sekretarieti ya TFF kuwasiliana na benki ya CRDB inayoendesha mfumo huo wa matumizi ya tiketi za elektroniki kuhusu upungufu huo na kuhakikisha unafanyiwa kazi.
MAREKEBISHO YA KATIBA YA TFF
Kamati ya Utendaji ya TFF imerejea mazungumzo kati yake na ujumbe wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) uliokuwa nchini ukiongozwa na Meneja wa Vyama Wanachama wa FIFA, James Johnson.  
Mazungumzo hayo kuhusu Katiba ya TFF yalifanyika Desemba 18 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Kamati ya Utendaji inasubiri rasimu ya Katiba hiyo kutoka FIFA ili iweze kufanya utaratibu wa kuwaarifu wanachama wake juu ya maudhui ya rasimu hiyo.
Shughuli ya FIFA kurekebisha katiba za nchi wanachama wake inaendelea duniani kote, na kwa Afrika kazi hiyo imekamilika katika nchi za Namibia, Zimbabwe na Malawi.
USHIRIKIANO KATI YA TFF NA SAFA
Kamati ya Utendaji imepitia na kupitisha makubaliano ya ushirikiano kati ya TFF na Chama cha Mpira wa Miguu Afrika Kusini (SAFA).
Makubaliano hayo ni ushirikiano katika nyanja za mpira wa miguu wa vijana, maendeleo ya waamuzi, ufundi, menejimenti ya matukio (event management) na utafutaji udhamini (sponsorship).
KANUNI ZA LESENI ZA KLABU (CLUB LICENSING REGULATIONS)
Kamati ya Utendaji imejadili rasimu ya Kanuni za Leseni za Klabu (Club Licensing Regulations), na kuagiza Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ifanye marekebisho ya mwisho, kabla ya kanuni hizo kusainiwa na kuanza kutumika.
UANZISHAJI MFUKO WA MAENDELEO YA MPIRA WA MIGUU (FDF)
Kamati ya Utendaji imepokea taarifa ya maendeleo ya mchakato wa uanzishwaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (Football Development Fund- FDF).
Imeipongeza Kamati ya Mfuko huo inayoongozwa na Rais wa zamani wa TFF, Leodegar Tenga, na kuitaka fanye jitihada za kukamilisha rasimu ya kanuni za uendeshaji mfuko huo.
Mbali ya Tenga, wajumbe wengine wa mfuko huo ni Ayoub Chamshama, Ephraim Mafuru, Frederick Mwakalebela, Tarimba Abbas na Zarina Madabida. Sekretarieti ya mfuko huo inaundwa na Henry Tandau ambaye ni Katibu, Wakili Emmanuel Muga na Boniface Wambura.
FDF ambao ni mfuko utakaokuwa unajitegemea utakuwa unashughulika na maendeleo ya mpira wa miguu kwa vijana, na nyanja nyingine za maendeleo kwa mchezo huo.
MKUTANO MKUU KUFANYIKA SINGIDA MACHI 14
Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imepanga Mkutano Mkuu wa Kawaida wa mwaka ufanyike Machi 14 na 15 mwakani mjini Singida.
MGOGORO NDANI YA ZFA
Kamati ya Utendaji imepokea kwa masikitiko taarifa za masuala ya mpira wa miguu Zanzibar kupelekwa mahakamani.
Kwa mujibu wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kitendo hicho ni kinyume cha taratibu za uendeshaji mpira wa miguu ambazo zinakataza masuala ya mchezo huo kupelekwa katika mahakama za kawaida.
Kamati ya Utendaji inatoa rai kwa pande zote mbili zinazohusika na mgogoro huo kukaa kwenye meza ya mazungumzo ili kumaliza tofauti zao. Kamati ya Utendaji imejitolea kutuma ujumbe wake Zanzibar ili ukutane na pande zinazohusika katika mgogoro huo.Ni muhimu usuluhisho upatikane haraka ili tuweze kujua hatma ya washiriki wetu kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi.

WANAHABARI WATEMBELEA GEREZA KUU LA WANAWAKE KINGOLWIRA – MOROGORO, WAMPONGEZA KAMISHNA JENERALI MINJA KWA JUHUDI KUBWA ZA MABORESHO NDANI YA MAGEREZA NCHINI

unnamed
unnamed1
Wafungwa wa kike wa Gereza Kuu la Wanawake Kingolwira – Morogoro wakifuma mashuka katika Kiwanda cha Ushonaji cha Gereza hilo. Wafungwa hao wanapitiwa ujuzi wa aina mbalimbali ikiwemo Ushonaji wa nguo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Programu za Urekebishaji ndani ya Magereza hapa nchini.
unnamed2
Muonekano wa mashuka na mito yake yanayofumwa na Wafungwa Wanawake katika Kiwanda cha Ushonaji cha Gereza Kuu la Wanawake Kingolwira – Morogoro.
unnamed3
Wanahabari wakionja chakula cha Wafungwa katika Gereza Kuu la Wanawake Kingolwira – Morogoro walipotembelea Gereza hilo Desemba 19, 2014(kulia) ni Mwandishi kutoka Gazeti la Habari Leo, Bi. Regina Kumba(kushoto) ni Mwandishi kutoka Gazeti la Daily News, Bw. Finning Simbeye(katikati) ni Mwanahabari kutoka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa, Bi. Rose Mdami
unnamed4
Mkuu wa Gereza Kuu la Wanawake Kingolwira – Morogoro, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Loyce Ruhembe akipokea rasmi msaada wa vitu mbalimbali vilivyotolewa na Wanahabari hao kwa ajili ya Wafungwa wa kike gerezani hapo walipotembelea Gereza hilo Desemba 19, 2014.
unnamed5
Mkuu wa Gereza Kuu la Wanawake Kingolwira – Morogoro, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Loyce Ruhembe akikabidhi msaada huo kwa Mfungwa wa Kike ambaye ndiye Nyampara Mkuu wa Gereza Kuu la Wanawake Kingolwira – Morogoro. Wafungwa wa Gereza hilo wamewashukru Wanahabari hao kuwatembelea pamoja na msaada huo walioutoa na wameahidi kuwa raia wema mara wamalizapo vifungo vyao.
unnamed6
Msaada wa vitu mbalimbali vya Kibinadamu na vinavyoruhusiwa Magerezani vilivyokabidhiwa na Wanahabari walipotembelea Gereza Kuu la Wanawake Kingolwira – Morogoro Desemba 19, 2014.
unnamed7
Mkuu wa Gereza Kuu la Wanawake Kingolwira – Morogoro, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Loyce Ruhembe(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wanahabari walipotembelea Gereza hilo Desemba 19, 2014. Wa tatu kushoto ni Mkuu wa Magereza Mkoani Morogoro, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Kato Rugainunula(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).