Wabunge
wa Kenya wametofautiana pakubwa bungeni kufuatia mjadala kuhusu mswaada
tatanishi wa usalama ambao wabnunge w aupinzani wanasema unakiuka uhuru
wa wakenya.
Bunge lililazimika kuahirisha vikao vyake kwa dakika
30 badala ya kujadili mswada tatanishi kuhusu usalama wa nchi. Kikao cha
leo kilikuwa kikao maalum ambacho kilipaswa kupitisha mswada huo ambao
baadaye utaidhinishwa na Rais kuwa sheria.
Wabunge wa upinzani wlaipinga mswada huo na kuanza kurusha karatasi sakafuni huku wakitatiza shughuli bungeni humo.
Mwenyekiti
wa kamati ya usalama wa bunge, Bwana Asman Kamama, alijaribu kuyaja
mabadiliko yaliyopendekezwa kufanyiwa mswada huo lakini wabunge walianza
kuimba na kumzomea spika wa bunge wakiukataa mswada huo wakisema 'bado
mapambano.'
Spika wa bunge Justin Muturi wakati mmoja alimuru
walinzi wa bunge kuwaondoa baadhi ya viongozi waliofika bungeni humo kwa
mjhadala ambao ulitarajiwa kuwa kaa moto, hasa kw aupande wa upinzani.
Mswada
huo ambao umewasilishwa bunge kufuatia matukio ya utovu wa usalama na
mashambulizi nchini Kenya, unapendekeza kuwa washukiwaw augaidi wanaweza
kuzuiliwa kwa mwaka mmoja huku polisi wakifanya uchunguzi.
No comments:
Post a Comment