Na Kibada Kibada-Katavi.
Dereva wa Pikipiki Maarufu kwa
jina la Bodaboda ameuwawa kwa kuchomwa kisu tumboni na abilia
aliyekuwa amembeba lengo la kutaka kupora Pikipiki.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa
Katavi Kamishina Msaidizi wa Polisi Dhahari Kidavashari ameleza katika
Taarifa yake kwa vyombo vya Habari kuwa alimtaja aliyeuwawa kuwa ni
Zakari Lungwa (24) mkazi wa Kawajense Mjini Mpanda.
Kamanda alieleza kuwa tukio hilo
limetoea Usiku wa kuamkia leo Disemba 15 majira ya saa sita na robo
usiku huko maeneo ya Kichangani Kata ya Nsemulwa Tarafa ya Kashaulili
Wilaya ya Mpanda .
Alisema kuwa huyo kijana
Zacharia alivamiwa na watu wawili anaowafahamu kwa sura na kumpora
pikipiki aina ya sanya nyekundu na kisha kumchoma kisu tumbon
na kusababisha mauti yake.
Ameeleza katika taarifa yake kuwa pamoja na marehemu kupiga kelele lakini hakufanikiwa kupata msaada mpaka mauti kumfika.
Aidha Kamanda amewashauri
madereva wanapopata abiria nyakati za usiku basi wawe wawili ili
waweze kusaidiana kama tatizo likijitokeza.
Katika tukio hilo Jeshi la
Polisi linamshikilia mtu mmoja Mwenye asilia ya Kiasia aliyefahamika
kwa jina la Khalidi Self Mwarabu miaka (24),mkazi wa Nsemulwa.
Jeshi la Polisi linaendelea
na upelelezi ili kubaini mtuhumiwa na kumtia mbaloni mtuhumiwa wa
mauaji hayo na wote wanaohusika.
No comments:
Post a Comment