Jokate Mwegelo akizungumza katika hafla hiyo
Jokate na Guoxun wakibadilishana mikataba baada ya kusaini
Jokate na Guoxun wakionyesha mikataba baada ya kusaini
Afisa Mtendaji mkuu wa kampuni ya Rainbow Shell Craft Company Limited (CEO), Deng Guoxun akuzungumza katika hafla hiyo
Wageni mbalimbali waalikwa wakishughudia hafla hiyo
Jokate akiteta jambo na Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa kwenye hafla hiyo
…………………………………………………………………………………………..
Na Mwandishi wetu
Dar es Salaam. Mbunifu mavazi,
Miss Tanzania wa namba mbili 2006, mwanamuziki na muigizaji wa filamu,
Jokate Mwegelo amesaini makubaliano yenye thamani ya Sh8.5 billion na
kampuni ya Kichina, Rainbow Shell Craft Company Limited kwa ajili ya
kuzalisha na kuuza bidhaa mbalimbali za lebo yake ya Kidoti.
Makubaliano hayo yalisainiwa
jana kwenye hotel ya Serena baina ya Jokate na Afisa Mtendaji mkuu wa
kampuni ya Rainbow Shell Craft Company Limited (CEO), Deng Guoxun.
Akizungumza katika hafla hiyo,
Jokate alisema kuwa makubaliano hayo ni ya kudumu na kampuni hizo mbili
zitazalisha na kuuza bidhaa za kidoti Tanzania nzima na nje ya mipaka
yake.
Alifafanua kuwa kampuni ya China
itawekeza Tanzania na kuwafaidisha watanzania kwa kutoa nafasi ya
ajira. Alisema kuwa pia wanatarajia kujenga kiwanda ili kuinua uchumi wa
nchi na maisha ya watanzania.
“Hii ni hatua kubwa ya
maendeleo kwangu, kama unavyojua, wakati naanza kujishugulisha na
masuala ya urembo, ubunifu na uanamitindo, sikutegemea kufikia hatua hii
ya kuingiza bidhaa zangu kimataifa, lakini sasa, ndoto zangu zimetimia
na najivunia mafanikio haya,” alisema Jokate.
Alisema kuwa mbali ya kutoa
mitindo tofauti ya kisasa ya nguo, kampuni yake pia itazalisha aina
mbali mbali za viatu, nywele ikiwa pamoja na mawigi, weaving, Rasta na
viatu vya wazi (sandals) ambazo kwa sasa zipo tayari kwenye soko la
Tanzania.
“Mpango wangu ni kupanua soko la
bidhaa zangu kama Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda, Afrika Kusini na nchi
nyingine za Afrika,” alisema.
Afisa Mtendaji wa Guoxun alisema
kuwa wamefurahi kukamilisha ubia na kampuni ya Kidoti na haya ni
matunda ya ushirikiano wa kudumu baina ya serikali yao na Tanzania.
“Tumefurahi sana kukamilisha
makubaliano haya, tunatarajia kuongoza katika soko la hapa nchini na
wenzetu (wachina) watafaidika pia, ” alisema Guoxun.
No comments:
Post a Comment