Wafungwa
wa kike wa Gereza Kuu la Wanawake Kingolwira – Morogoro wakifuma
mashuka katika Kiwanda cha Ushonaji cha Gereza hilo. Wafungwa hao
wanapitiwa ujuzi wa aina mbalimbali ikiwemo Ushonaji wa nguo ikiwa ni
sehemu ya utekelezaji wa Programu za Urekebishaji ndani ya Magereza hapa
nchini.
Muonekano
wa mashuka na mito yake yanayofumwa na Wafungwa Wanawake katika Kiwanda
cha Ushonaji cha Gereza Kuu la Wanawake Kingolwira – Morogoro.
Wanahabari
wakionja chakula cha Wafungwa katika Gereza Kuu la Wanawake Kingolwira –
Morogoro walipotembelea Gereza hilo Desemba 19, 2014(kulia) ni
Mwandishi kutoka Gazeti la Habari Leo, Bi. Regina Kumba(kushoto) ni
Mwandishi kutoka Gazeti la Daily News, Bw. Finning Simbeye(katikati) ni
Mwanahabari kutoka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa, Bi. Rose Mdami
Mkuu
wa Gereza Kuu la Wanawake Kingolwira – Morogoro, Mrakibu Mwandamizi wa
Magereza, Loyce Ruhembe akipokea rasmi msaada wa vitu mbalimbali
vilivyotolewa na Wanahabari hao kwa ajili ya Wafungwa wa kike gerezani
hapo walipotembelea Gereza hilo Desemba 19, 2014.
Mkuu
wa Gereza Kuu la Wanawake Kingolwira – Morogoro, Mrakibu Mwandamizi wa
Magereza, Loyce Ruhembe akikabidhi msaada huo kwa Mfungwa wa Kike ambaye
ndiye Nyampara Mkuu wa Gereza Kuu la Wanawake Kingolwira – Morogoro.
Wafungwa wa Gereza hilo wamewashukru Wanahabari hao kuwatembelea pamoja
na msaada huo walioutoa na wameahidi kuwa raia wema mara wamalizapo
vifungo vyao.
Msaada
wa vitu mbalimbali vya Kibinadamu na vinavyoruhusiwa Magerezani
vilivyokabidhiwa na Wanahabari walipotembelea Gereza Kuu la Wanawake
Kingolwira – Morogoro Desemba 19, 2014.
Mkuu
wa Gereza Kuu la Wanawake Kingolwira – Morogoro, Mrakibu Mwandamizi wa
Magereza, Loyce Ruhembe(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na
Wanahabari walipotembelea Gereza hilo Desemba 19, 2014. Wa tatu kushoto
ni Mkuu wa Magereza Mkoani Morogoro, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Kato
Rugainunula(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
No comments:
Post a Comment