Mkurugenzi wa Idara ya Uboreshaji Afya kutoka Taasisi ya Wamnawake na
Maendeleo, WAMA, Dkt. Sarrah Maongezi akiwasilisha mada kwenye mkutano
maalum wa wadau mbalimbali wa usonji (Autism) uliofanyika jijini Dar es
Salaam tarehe 16.12.2014 ili kuzungumzia hali halisi ya tatizo la usonji
na changamoto zake hapa nchini ili kujenga mfumo bora wa huduma kwa
watoto wenye usonji.
Daktari Kissah Mwambene kutoka Chama cha Madaktari wa Afya ya Akili
(MEHATA) akitoa uzoefu wa chama chao katika kushughulikia masuala ya
watoto walio na usonji hapa nchini kwenye mkutano wa wataalam na wadau
wa ugonjwa huo uliofanyika\ tarehe 16.12.2014. Makamu
wa Rais Mwandamizi Profesa Andy Shih anayeshughulikia masuala ya
sayansi kutoka Shirika la Kimataifa linaloshughulikia uboreshaji wa
huduma kwa watu wenye matatizo ya usonji duniani,( Autism Speaks) akitoa
taarifa kuhusu shughuli na miradi ya Shirika hilo lenye makao makuu
yake New York nchini Marekani.
Katibu wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Ndugu Daud Nassib
akiongoza majadiliano kwenye mkutano wa wataalam na wadau wa Usonji
uliofanyika jijini Dar es Salaa tarehe 16.12.2014. Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, Mama Salma
Kikwete akimkaribisha kwa mazungumzo Profesa Andy Shih, Makamu wa Rais
Mwandamizi kutoka Shirika la Autism Speaks aliyemtembelea Mama Salma
ofisini kwake tarehe 17.12.2014. Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akizungumza na
wajumbe wa mkutano maalum ulioandaliwa na Taasisi yake kuhusu tatizo la
hapa nchini. Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akizungumza na
wajumbe wa mkutano maalum ulioandaliwa na Taasisi yake kuhusu tatizo la
hapa nchini.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Makamu wa Rais
Mwandamizi Profesa Andy Shih anayeshughulikia masuala ya sayansi kutoka
shirika la Autism Speaks lenye Makao Makuu yake huko New York nchini
Marekani. Profesa Shih akifuatana na Dkt. Kra Reagan walimtembelea Rais
Kikwete huko Ikulu tarehe 17.12.2014. Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Dkt. Kra Reagan katikati ni Makamu
wa Rais Mwandamizi Profesa Andy Shih anayeshughulikia masuala ya
sayansi kutoka shirika la Autism Speaks lenye Makao Makuu yake huko New
York nchini Marekani. Profesa Shih akifuatana na na Dkt. Kra Reagan walimtembelea Rais Kikwete huko Ikulu tarehe 17.12.2014. Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akifanya mazungumzo na Profesa Andy Shih aliyemtembelea huko Ikulu tarehe 17.12.2014.
PICHA NA JOHN LUKUWI.
No comments:
Post a Comment