Mkuu wa operesheni wa Benki ya Exim, Bw. Eugen Massawe (kushoto)
akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika mkutano na
vyombo vya habari uliofanyika Dar es Salaam, jana, kuzindua ‘Exim Smart
App’, program ya simu iliyotengenezwa maalumu kwa ajili ya simu aina ya
‘smartphones’ itakayowawezesha wateja wa benki hiyo kupata huduma za
kibenki kupitia simu zao za mkononi. Kulia ni Afisa Masoko wa benki
hiyo, Noel Tuga.
Katika jitihada zake za kuboresha utoaji wa huduma za kibenki kupitia
simu za mkononi, Benki ya Exim imezindua program mpya ya simu ya aina
yake kwa wateja wa benki hiyo wanaotumia simu aina ya ‘smart phone’.
Programu hiyo kwa sasa inapatikana katika simu zilizo na uwezo wa Android, Windows, Black Berry na mfumo wa IOS.
Akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam jana, Mkuu wa Operesheni wa Benki ya Exim, Be. Eugen Massawe alisema kuwa programu hiyo mpya inatoa fursa kwa wateja wa benki hiyo kufurahia huduma salama za kibenki kupitia simu zao za mkononi kama vile kuangalia miamala, kupokea taarifa za akaunti katika zao pamoja na huduma nyingine nyingi.
“Kwa kupitia Exim Smart App, sasa wateja wa Benki ya Exim wataweza kuangalia taarifa mbalimbali zinazohusu akaunti zao na kufuatilia miamala yote itakayokuwa ikifanyika kwenye akaunti zao kwa urahisi zaidi.
“Programu yetu ya simu ni rahisi sana kutumia ikiwa imeundwa kwa kumzingizatia mteja ili kumuwezesha kuona machaguo mbalimbali punde tu anapoifungua programu hii na hili limefanyika hili kupunguza mlolongo mrefu katika uchaguzi wa huduma ambayo mteja atakuwa anahitaji,” alisema Bw. Massawe.
Bw. Massawe alisema kuwa Benki ya Exim imekuwa benki ya kwanza ya kitanzania kutambulisha programu ya aina hiyo, jambo lililotokana na juhudi za makusudi zinazofanywa na benki hiyo ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wateja wake.
“Mteja atahitajika kuwa amejisajiliwa na ‘Exim Mobile Banking’ ili kuweza kutumia program hii mpya ya Exim Smart App itakayomuwezesha kufurahia ulimwengu mpya wa kibenki.
Lengo letu ni kuwawezesha wateja wetu kufanya biashara zao kwa urahisi zaidi, kwa njia yoyote ile wanayopendelea, aidha kupitia kompyuta za mezani au kupitia simu zao za mkononi,” aliongeza.
Huduma za kibenki kupitia simu za kiganjani zimeendelea kupata umaarufu mkubwa, huku wateja wakionyesha kuvutiwa zaidi na njia hii mpya inayowawezesha kufanya miamala pasipo ulazima wa kutembelea tawi la benki.
Exim Smart App inapatikana bure na inaweza kupakuliwa kutoka kwenye App Store.

No comments:
Post a Comment