Baadhi ya wananchi wakiwa
wamejipanga katika mistari wakisubiri kupiga kura katika uchaguzi wa
Serikali za Mitaa na vitongoji uliofanyika jumapili wiki iliyopita
jijini mkoani Katavi.
Baadhi ya wananchi akihakikiwa majina yao kabla ya kupiga kura mkoani Katavi.
………………………………………………………………………………..
Na Kibada Kibada –Katavi
KatikaUchaguzi uliomalizika wa
Serikali za Mitaa kwa hapa nchini kwa upande wa Halmashauri ya Wilaya
ya Mpanda Mkoa wa Katavi Chama cha Mapinduzi (CCM) kimepata ushindi kwa
kujizolea viti vya 138 katika nafasi ya kitongoji kati ya vitongoji 215
katika Halmashauri hiyo huku CHADEMA ikipata viti 62 na CUF viti
vitano.
Kwa mjibu wa Afisa Uchaguzi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Charles Linda ameeleza kuwa kwa matokeo
hayo chama cha mapinduzi kimepata ushindi wa asilimia 63.8 wakati Chama
cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA) kimepata asilimia 29.96 na Chama
cha wananchi ( CUF) kimepata asimilia 2.3.
Akizungumzia nafasi ya
Mwenyekiti wa Kijiji CCM imepata viti 26 na CHADEMA imepata viti vya
uenyekiti wa kijiji 15 na CUF imejinyakulia kiti kimoja.
Aidha Linda alieleza kuwa katika
uchaguzi huo ni kwa matokeo yaliyopokelewa kutoka kwenye maeneo
mbalimbali ya Halmashauri hiyo ingawa ilikuwa imebakia vitongoji vinane
ambavyo vilikuwa bado hawajawasilisha matokeo ambayo hayawezi kubadili
sura ya matokeo.
Na kuongeza kuwa katika
kitongoji kimoja wagombea wagombea wamegongana kwa kulingana kura
zilizohesabiwa mgombea wa chama cha Mapinduzi na Mgombea wa cha cha
Demokrasia na Maendeleo CHADEMA hivyo kwa mjibu wa taratibu Kanuni na
sheria itabidi uchaguzi urudiwe upya kadiri itakavyokuwa imepangwa.
Kwa upande wa matokeo ya awali
Halmashauri ya Mji wa Mpanda inaonesha kuwa pia CCM imepata viti 28
katika uchaguzi wa nafasi ya mwenyekiti wa Mitaa sawa na asilimia kati
ya 65 na 68 .
Kwa Mjibu wa matokeo ya awali
yaliyotolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mpanda Seleman Lukanga
yanaonesha kuwa Chama cha Demokrasi na Maendeleo CHADEMA kimepata
mitaa 13 sawa na asilimia kati ya 32 na 38Ameeleza kuwa hayo ni matokeo
ya awali matokeo kamili yatatolewa baada ya kukamilika kwa shughuli ya
kuhesabu na kuweka matokeo sawa ya vituo vyote.
Matokeo hayo ni yale
yaliyotolewa kwa Halamshauri ya Wilaya ya Mpanda na Halmashauri ya Mji
wa Mpanda wakati yale ya Halmashauri ya Mlele Na Halmashauri ya Wilaya
ya Nsimbo walikuwa bado hawajatoa matokeo.
Hata hiyo katika uchaguzi huo
kulijitokeza changamoto za hapa na pale ambazo zilipatiwa ufumbuzi na
uchaguzi ukafanikiwa kufanyika na kuenda vizuri karibu maeneo yote
Halmashauri hizo.
Kwa upande wa matokeo ya
Halmashauri ya Nsimbo na Halmashauri ya Mlele kulikuwa pado matokeo
kupatikana kulinga na jiografia ya maeneo ya vijiji na maeneo mengine
walikuwa bado hawajakamilisha matokeo yataendelea kutolewa pindi
yatakapoendelea kutolewa.
No comments:
Post a Comment