KAMPUNI ya Simu Tanzania (TTCL)
imezinduwa huduma mpya kabambe ambayo inampa mteja wa kapuni hiyo fursa
ya kufurahia modem ya bure na vifurushi vya intaneti kwa bei nafuu,
huduma ambayo imetolewa kama ofa kwa wateja hasa katika kuelekea siku
kuu za Chrismas na Mwaka mpya.
Akizungumza leo jijini Dar es
Salaam juu ya huduma hiyo, Meneja Huduma za Intaneti wa TTCL, Abdul
Mombokaleo amesema kampuni ya Simu Tanzania imeamua kuzindua promosheni
mpya ya “DILI LA UKWELI” inayotoa fursa ya mteja wa TTCL kufurahia
huduma ya intaneti kwa bei nafuu zaidi na kujipatia modem.
“…TTCL siku ya leo imezindua
promosheni mpya ya “DILI LA UKWELI” inayotoa fursa ya mteja wa TTCL
kufurahia huduma ya intaneti kwa bei nafuu zaidi na kujipatia modem ya
bure.
Akifafanua zaidi Mambokaleo
alisema promosheni hiyo mpya ya “Dili la Ukweli” inatoa fursa kwa wateja
kufurahi modem ya bure pamoja na vifurushi ambavyo vimepunguzwa bei kwa
kiwango ambacho Mtanzania wa kawaida anaweza kuimudu.
Aidha akifafanua juu ya
utaratibu wa promosheni alisema ili mteja apate modem ya bure Mteja
atapaswa kununua intaneti bila kikomo kwa shilingi 20,000/- tu ambayo
itatumika ndani ya mwezi mzima na huduma hiyo ni kwa wateja wapya tu.
“…Kwa mteja wenye modem tumewapa
fursa ya kuchagua vifurushi ambavyo vimepunguzwa bei. DILI LA UKWELI
inatoa fursa kwa wateja kufurahia punguzo la bei ya vifurushi vya
intaneti vya siku, wiki na mwezi kwa bei nafuu sana. Intaneti ya TTCL
inaubora, ina kasi na uwakika, kwani teknolojia inayotumika ni ya
kuaminika zaidi. Katika kuhakikisha wateja wa huduma ya intaneti
wanafurahia zaidi, TTCL imeshusha bei ya intaneti ili kuendelea kukidhi
mahitaji ya wateja wake.
No comments:
Post a Comment