Wageni mbalimbali wanaoshiriki
mkutano mkubwa wa kimataifa wa hifadhi ya jamii ulioandaliwa na
serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Fedha ulioanza leo katika kituo
cha kimataifa cha mikutano cha Arusha (AICC) wakifanya usajili kabla ya
kuanza kwa mkutano huo. (Picha zote na Zainul Mzige wa MOblog).
Na Mwandishi wetu
MAKAMU wa pili wa rais Zanzibar
Balozi Seif Ali Iddi, amesema mpango wa serikali ya Tanzania wa hifadhi
ya jamii ndio msingi wa sera ya kuondoa umaskini miongoni mwa watu wake
ili kulifanya taifa kuwa la kipato cha kati ifikapo 2025.
Kauli hiyo imetolewa leo wakati
akifungua mkutano mkubwa wa kimataifa wa hifadhi ya jamii ulioandaliwa
na serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Fedha na wadau wengine kwa
lengo la kubadilishana uzoefu juu ya nini cha kufanya kusaidia makundi
maalumu katika jamii.
Katika Mkutano huo wa siku tatu
unafanyika Katika kituo cha kimataifa cha mikutano cha Arusha (AICC)
serikali imefanya maandalizi kwa kushirikiana na mashirika ya kimataifa
kama UNICEF, ILO, UNAIDS na taasisi ya utafiti wa sera za kiuchumi
yenye makao makuu nchini Afrika Kusini (EPRI).
Imeelezwa kuwa mkutamo huo
umelenga kuchota maarifa mema kutoka Afrika Kusini ya namna ya
kutengeneza sera za kuhudumia makundi maalumu ya wanawake, watoto,
wazee, wasiojiweza na vijana ili kuboresha maisha yao, ikiwa ni sehemu
ya mpango mkakati wa serikali wa kuinua kiwango cha maisha miongoni mwa
wananchi wake.
Mkurugenzi msaidizi Mkuu wa
Shirika la Kazi duniani na Mkurugenzi wa kanda ya Afrika Aeneas C. Chuma
(kulia) akiwasili kushiriki mkutano huo akiwa ameambatana na Afisa
Habari wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) Tanzania, Bw. Magnus Minja
(kulia) pamoja na Luis Frota kutoka ILO Afrika Kusini.
Balozi Seif Ali Iddi, alisema kwa
kuzingatia nia ya serikali ya kuwa taifa lenye kipato cha kati mwaka
2025 serikali inaona haja ya kuangalia sera ili iweze kutoa haki kwa
makundi yote kuelekea ustawi wa jamii ifikapo mwaka huo..
“Serikali imechukua hifadhi ya
jamii kama mkakati wa kufikia dira ya ukuaji na maendeleo nchini.
Kongamano hili limekusudia kuhakikisha kwamba muono unatengeneza hatua
stahiki zinazotekelezeka kitaifa kukabiliana na changamoto za umaskini
hivyo kuhakikisha ukuaji wa uchumi unakuwa endelevu na wenye maana kwa
wananchi” alisema.
Alisema ili kufikia lengo hilo la
uchumi endelevu, serikali inataka kuhakikisha wananchi wake wakiwemo
wale maskini na wasiojiweza wanawezeshwa ili kutambua haki zao na
kuifanya Tanzania kuwa taifa lenye nguvu na linalotoa haki sawa kwa
wote.
Aidha kuwa taifa linaloangalia
mahitaji ya watoto wake kama lishe, afya na elimu ili kuwasaidia kukua
kwa furaha, kuwa wazalishaji na kukwepa mtego wa umaskini unazinga
kizazi kwa kizazi.
Mtaalam wa Mahusiano na
Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania Hoyce Temu (kulia)
akimwongoza Mkurugenzi msaidizi Mkuu wa Shirika la Kazi duniani na
Mkurugenzi wa kanda ya Afrika Aeneas C. Chuma kuelekea kwenye chumba
maalum cha wageni mashuhuri kabla ya kuanza kwa mkutano. Katikati
ni Afisa Habari wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) Tanzania, Bw. Magnus
Minja.
Balozi Iddi alisema kwamba
amefurahi kuona kwamba ajenda za mkutano pia zimegusia kuzungumzia
uimarishaji wa utendaji wa pamoja kati ya mipango ya hifadhi ya jamii
kama TASAF, Mfuko wa afya ya jamii (CHF) na huduma za jamii zinazotolewa
na wizara husika kama wizara ya elimu, afya, maji nakadhalika.
Hata hivyo aliwataka washiriki
kuangalia ukusanyaji wa takwimu kuhusu masuala ya hifadhji ya jamii
kwani kwa hali ilivyo sasa ukusanyaji huo si mzuri na unazuia maendeleo
na uimarishaji wa huduma za jamii.
Alisema ipo haja ya kuboresha
mazingira ya utawala ili kuwezesha kuimarisha hifadhi kwa wale
waliokwishaipata, kubadili sheria ili kuwaingiza na wale ambao
hawajapata huduma za hifadhi ya jamii.
Aliwataka washiriki kuangalia kwa makini changamoto zinazoikumba Afrika na Tanzania katika masuala ya hifadhi na kutolea majibu.
Mratibu Mkazi wa mashirika ya
Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa
Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kulia) akisalimiana
na Mkurugenzi msaidizi Mkuu wa Shirika la Kazi duniani (ILO) na
Mkurugenzi wa kanda ya Afrika Aeneas C. Chuma.
Alizitaja baadhi ya changamoto
hizo kuwa ni umaskini uliotapakaa ambao unasababisha watu kushindwa
kupeleka michango katika hifadhi, misingi ya ukataji kodi ambayo huleta
mushkeri kwa fedha za hifadhi, kuwepo kwa kundi kubwa lisilo katika
sekta rasmi ya ajira na hivyo kupunguza idadi ya wachangaji katika
prgramu zinazohitaji michango mfululizo na mabadiliko ya tabia nchi
yanayotishia kuyumba kwa kilimo na ufugaji ambao ndio msingi wa mapato
kwa wananchi wengi.
Alisema pia mabadiliko ya tabia
nchi yanasababisha milipuko ya magonjwa mbalimbali kama Malaria na
magonjwa mengine mapya kama Ebola na Dengue.
Changamoto nyingine ni kuwepo na gharama kubwa za utawala hasa katika siku za mwanzo za uanzishwaji wa mifuko ya hifadhi.
Mkutano huo wenye washiriki zaidi
ya 150 una watu wa kariba mbalimbali wakiwemo watengeneza sera, watafiti
na waendeshaji wa mifuko ya hifadhi kutoka mataifa ya Kenya, Uganda,
Bangladesh, Mozambique, Lesotho, Malawi, Afrika Kusini, Ghana, Ethiopia,
Zambia, Sudan Kusini na wenyeji Tanzania.
Mratibu Mkazi wa mashirika ya
Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa
Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto) akibadilishana mawazo
na Mkurugenzi msaidizi Mkuu wa Shirika la Kazi duniani na Mkurugenzi wa
kanda ya Afrika Aeneas C. Chuma kabla ya kuwasili kwa mgeni rasmi Balozi
Seif Ali Iddi.
Mkutano huo unatarajiwa kutoa
mwelekeo wa namna ambavyo Tanzania inaweza kuanzisha mfumo wa hifadhi
kwa ajili ya watu maskini na wale wenye mahitaji maalumu ili kuwawezesha
kupata huduma za afya, elimu na kipato.
Naye Mkurugenzi msaidizi Mkuu wa
Shirika la Kazi duniani na Mkurugenzi wa kanda ya Afrika Aeneas C.
Chuma, amesema Umoja wa Mataifa umefurahishwa na kuwapo kwa kongamano
hilo kwani suala la hifadhi ni msingi wa maendeleo katika uchumi wowote
endelevu.
Alisema kuwapo kwa Hifadhi ya
jamii inayoeleweka na yenye msingi imara husaidia wananchi kukabiliana
na mabadiliko yoyote yale ya kiuchumi katika taifa lao.
Alisema shirika hilo katika miaka
yote 95 ya uwapo wake inapigania hifadi ya jamii kama njia salama ambayo
inahakikisha ukuaji wa jamii unaozingatia uwapo wa jamii inayozingatia
ukuaji wa uchumi wenye haki kwa kila mmoja.
Waziri wa Fedha, Mh. Saada
Mkuya Salum (kushoto) akiwasili kwenye viwanja vya AICC jijini Arusha
kushiriki mkutano mkubwa wa kimataifa wa hifadhi ya jamii ulioandaliwa
na serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Fedha huku akiwa ameongozana
na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dr. Servacius Likwelile (katikati)
pamoja na Mwakilishi wa UNICEF Tanzania, Jama Gulaid.
Pamoja na mafanikio ya dunia
katika masuala ya afya na elimu, Mwakilishi huyo ameelezea changamoto
kubwa inayokabili Tanzania ambayo ni vijana wengi kuingia katika soko la
ajira ambalo ni finyu.
Mwakilishi huyo amesema kwamba
kuanzia mwaka ujao hadi 2030 nchi za Afrika Kusini mwa jangwa la
sahara wanatakiwa kutengeneza nafasi milioni 5 za kazi kila mwaka ili
kuendana na ukuaji wa soko la wasaka ajira.
Alisema kutokana na ukweli huo
hatua ya sasa ya Tanzania kutaka kuwa na msingi imara ya hifadhi ya
jamii ni muhimu sana ili kukabiliana na mabadiliko yanayokuja katika
afya, elimu na ajira.
Wakati huo huo Mratibu wa
mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mkurugenzi mkazi wa UNDP Alvaro
Rodriguez amesema hifadhi ya jamii ni kitu muhimu kinachofanya
watengeneza sera kukaa pamoja kuona namna nzuri ya kufanikisha masuala
hayo.
Waziri wa Fedha, Mh. Saada
Mkuya Salum (katikati) akiwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Mhe. Dkt. Shukuru Kawambwa (kushoto) pamoja na Naibu waziri wa Maendeleo
ya Jamii, Jinsia na Watoto Mhe. Dkt. Pindi Chana wakielekea kumpokea
mgeni rasmi Makamu wa pili wa rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,
Balozi Seif Iddi.
Alisema matukio mbalimbali
yanayoharibu ustawi wa jamii kama kuporomoka kwa uchumi duniani,
mabadiliko kwenye tabianchi kumefanya kuwepo na haja ya kuhakikisha
kwamba kuna misingi imara ya kutoa hifadhi kwa wananchi na kuboresha
maisha yao.
Akizungumza katika mkutano huo kabla ya Makamu wa rais kuhutubia, Alvaro alisema kuna changamoto kubwa zinazokabili dunia.
Alipongeza serikali ya Tanzania
kwa kuona haja ya kushirikiana na wadau wengine kuona namna bora ya
kukabiliana na changamoto za maendeleo katika lengo la kuhakikisha
kunauwezeshaji wenye lengo la kuwezesha ustawi wa jamii.
Alisema mada zitakazojadiliwa
zitawezesha mwishoni mwa mkutano kuwapo na maazimio yenye kuwezesha
kutengenezwa kwa mising bora ya hifadhi ya jamii ili kuwezesha maono ya
maendeleo kufikiwa.
Mratibu huyo pia alielezea
kuridhishwa kwake na mafanikio yanayopatikana nchini Tanzania kupitia
TASAF ya kukabiliana na umaskini uliokithiri na kutoa nafasi ya maskini
kuwa na uwezo wa kusonga mbele katika maendeleo ili kufikia maono ya
taifa ya maendeleo endelevu yanayojali watu wote 2025 wakati taifa
litakapokuwa la kipato cha kati.
Mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa
mkutano mkubwa wa kimataifa wa hifadhi ya jamii ulioandaliwa na
serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Fedha, Makamu wa pili wa rais wa
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Iddi akisalimiana na Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dr. Servacius Likwelile mara baada ya kuwasili
kwenye viwanja vya AICC jijini Arusha leo.
Makamu wa pili wa rais wa
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Iddi , akisalimiana
na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa
Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez
alipowasili kwenye ufunguzi wa mkutano wa kimataifa wa hifadhi ya
jamii.
Mgeni rasmi Makamu wa pili wa
rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Iddi akisalimiana na
Mwakilishi wa Shirika la watoto duniani (UNICEF), Jama Gulaid.
Mgeni rasmi Makamu wa pili wa
rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Iddi (katikati)
akiwa na Waziri wa Fedha, Mh. Saada Mkuya Salum pamoja na mwenyeji wao
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda wakielekea kwenye ukumbi wa
mikutano.
Picha juu na chini ni mgeni
rasmi Makamu wa pili wa rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi
Seif Iddi, akifungua mkutano mkubwa wa kimataifa wa hifadhi ya jamii
ulioandaliwa na serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Fedha na wadau
wengine kwa lengo la kubadilishana uzoefu juu ya nini cha kufanya
kusaidia makundi maalumu katika jamii ulioanza leo jijini Arusha.
Kwa picha zaidi ingia humu
No comments:
Post a Comment