Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Ummy Mwalimu kushoto
akipata maelekezo mafupi toka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya OK
Plastic Bw.Fadl Ghaddar wakati alipofanya ziara ya kushtukiza kiwandani
hapo jijini Dar es Salaam ili kujionea hali halisi ya kiwanda hicho
katika kutunza mazingira, katikati ni Mkurugenzi Msaidizi wa Mazingira
toka Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Bi. Magdalena Mtenga.
Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Ummy Mwalimu
(katikati) akipata maelezo toka kwa Mkurugenzi Msaidizi wa Mazingira
toka Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Bi. Magdalena Mtenga wakati
alipofanya ziara ya kushtukiza katika kiwanda cha OK Plastic jijini Dar
es Salaam, kulia ni Meneja wa Kiwanda hicho Bw. Martin Msamba.
Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Ummy Mwalimu
(katikati) akimsikiliza kwa makini Mkuu wa Kitengo cha Uzingatiaji wa
Usimamizi wa Mazingira toka Baraza la Mazingira (NEMC) wakati alipofanya
ziara ya kushtukiza katika kiwanda cha OK Plastic Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Ummy Mwalimu
(katikati) akisistiza jambo kwa Meneja wa Kiwanda cha OK Plastic Bw.
Martin Msamba wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika kiwanda cha
OK Plastic jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa
Mazingira toka Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Bi. Magdalena Mtenga. Baadhi
ya wafanyakazi wa kiwanda cha OK Plastic ambao majina yao hayakuweza
kupatikana wakionekana kufanya kazi katika mazingira ambayo si rafiki
kwa afya zao.
Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Ummy Mwalimu akitoa
maelekezo kwa watendaji wa Baraza la Mazingira (NEMC) na uongozi wa
kiwanda cha OK Plasdtic juu ya hatua za haraka za kuchukua ili
kukabiliana na tatizo la uchafuzi wa mazingira jijini Dar es Salaam.
Picha zote na Eliphace Marwa – Maelezo
No comments:
Post a Comment