Naibu Waziri wa Maji,Mh Amos Makala akiongea na vyombo vya
habaria katika ziara yake ya kikazi jijini hapa kwa lengo la kutembelea
miradi ya maji iliyokuwa na changamoto kubwa ya upotevu wa maji
inayosababishwa na uchakavu wa miundombinu na wizi wa maji
Naibu
Waziri wa Maji,Mh Amos Makala kulia akiwa anasikiliza maelezo kutoka
kwa Eng wa maji Bw.Mohamed Ismail katika eneo la chanzo cha maji mto
nduruma katikati niKaimu mkurugenzi wa mamlaka ya maji Arusha Eng.Fabian
Maganga
Muonekano wa maporomoko ya maji mto nduruma ni chanzo kikubwa kinachotegemewa Mkoani Arusha katika huduma ya maji
Askari anayelinda eneo hilo
Naibu Waziri wa Maji,Mh Amos
Makala wa nne kulia akiwa anateta jambo katika moja ya maporomoko ya
maji ijulikanayo kama mto nduruma wengine ni watumishi wa mamlaka hiyo
Kulia aliyesimama ni Makamu
mwenyekiti wa bodi ya maji Mkoa wa Arusha Bw.Joshua Kileo akiwa
anazungumza wakati Naibu Waziri wa Maji,Mh Amos Makala alipokuwa
anazungumza na watumishi wa mamlaka ya maji Arusha leo
Naibu Waziri wa Maji,Mh Amos
Makala akiwa anaangalia moja ya ujenzi wa chanzo kipya cha maji katika
eneo la kisongo ambacho kitasaidia wananchi wa eneo hilo kupata huduma
ya maji
Hii ni mitambo ya kuwekea maji dawa
Naibu Waziri wa Maji,Mh Amos Makala akiangalia moja ya kisima cha maji katika kijiji cha Olturuto wilaya Arumeru
Naibu Waziri wa Maji,Mh Amos Makala akionge akatika moja ya chanzo cha maji kinachotengenezwa eno la kisongo Mkoa Arusha
Na Pamela Mollel wa jamiiblog
Naibu Waziri wa
Maji,Mh Amos Makala amewataka wananchi wa Mkoa wa Arusha kuendelea
kuwafichua wale wote wanaoshiriki katika wizi wa maji ili waweze
kuchukuliwa hatua kali za kisheria.
Alitoa wito huo jana wakati akiwa katika ziara yake ya kikazi
jijini hapa kwa lengo la kutembelea miradi ya maji iliyokuwa na
changamoto kubwa ya upotevu wa maji inayosababishwa na uchakavu wa
miundombinu na wizi wa maji
Waziri Makala alisema kuwa serikali inafanya jitihada ya
kuboresha huduma ya maji ikiwa nipamoja na kuboresha
miundombinu,kukomesha wizi wa maji kwa kutoa elimu kwa wananchi
“Wizi wa kujiunganishia maji katika maeneo mbalimbali hapa
nchini upo lakini kwa sasa tunaoparesheni ya kuwasaka wale wote
wanaotumia maji bila kulipa watambue kuwa kwa kufanya hivyo ni kinyume
na sheria”alisema Makala
Aidha katika moja ya chanzo kikubwa cha maji mto nduruma alisema
kuwa chanzo hicho kinategemewa kwa mkoa wa Arusha hivyo alitoa pongezi
kwa mamlaka ya maji kwa kuwa wabunifu
Naye Kaimu mkurugenzi wa mamlaka ya maji Arusha Eng.Fabian
Maganga alisema kuwa kwa hivi karibuni walikuwa na zoezi la ukaguzi wa
nyumba hadi nyumba na kufanikiwa kuwakamata watu wanaohujumu mamlaka
hiyo takribani 750 hivyo zoezi hilo bado ni endelevu
No comments:
Post a Comment