Msanii wa muziki wa kizazi
kipya Ney wa Mitego anatarajiwa kulipamba Tamasha la amani
linalotarajiwa kufanyika mapema jumamosi hii desemba 20 katika viwanja
vya Sheik Amri Abeid lililoko mkoani Arusha.
Akizungumza na waandishi wa
habari, mratibu wa Tamasha hilo Bertha Ismail kupitia kampuni ya Bimo
media alisema kuwa Msanii huyo anaetamba na wimbo wake wa “Nakula Ujana”
anatarajiwa kutua mkoani Arusha siku ya Alhamisi ya desemba 18 na timu
yake nzima ambapo atafanya matangazo katika sehemu mbalimbali za jiji la
Arusha kuhamasisha watu kuhudhuria tamasha hilo.
“Mbali na wasanii wengine wa
Arusha, Msanii mkubwa ambae anatarajiwa kulipamba tamasha hilo ni Ney wa
Mitego ambae tunaamini kwa Arusha atavuta watu wengi kuhudhuria tamasha
katika uwanja wa Sheik amri abeid kuja kusikiliza ujumbe wa Amani
ambapo utatolewa na Mgeni Rasmi”alisema Bertha.
Alisema kuwa Tamasha hilo
litakalohudhuriwa na viongozi mbali wa serikali, Tasisi pamoja vyama vya
siasa, lengo kubwa ni kuwaunganisha vijana na kupata ujumbe wa amani
hasa katika kipindi hiki tunapoelekea uchaguzi mkuu wa mwakani, ujumbe
utakaotolewa na msajili wa vyama vya siasa nchini Jaji Francis Mutungi.
“Tunapoelekea uchaguzi tunajua
mara nyingi sisi vijana ndio tunaotumika zaidi, hivyo lengo kuu la
Tamasha hili ni kuwaunganisha vijana katika umoja ili wasigawanywe kwa
misingi ya dini na siasa hali itakayojenga chuki na kufanyiana fujo,
hivyo wasifanye hivyo bali kila mmoja atumikie chama chake au dini yake
kwa amani bila vurugu”
Bertha alisema kuwa Tamasha
hilo lililodhaminiwa na kiwanda cha soda cha pepsi, Kituo cha redio five
na Sunrise Arusha, Mbali na Burudani ya Ney wa mitego pia kutakuwa na
burudani zingine kama Ngoma za asili, sarakasi, maonyesho ya warembo wa
mitindo pia vijana chipukizi wa Arusha wataimba nyimbo mbali mbali
sambamba na Watangazaji wa redio za Arusha kukimbia riadha hivyo kutumia
fursa hiyo kuwaalika wadhamini kutumia nafasi hiyo kutangaza bidhaa zao
kwa kushiriki tamasha hilo.
No comments:
Post a Comment