Kikosi cha Timu ya waandishi wa Habari nchini Tanzania(TASWA FC) leo kitashuka dimbani kukipiga dhidi ya timu ya kombaini ya Makipa wanaocheza ligi kuu ya Vodacom Tanzania, mchezo utakaopigwa kwenye Dimba la Uwanja wa Karume jijjini Dar es Salaam.
Akizungumzia mchezo huo mwenyekiti wa Taswa, Majuto Omary amesema kuwa mchezo huo ni wa kirafiki wenye lengo la kuweka Mahusiano mazuri baina ya waandishi na Makipa wanaocheza ligi kuu Ya Vodacom Tanzania.
"ni mchezo wa kirafiki ambao nadhani utakuwa ni kivutio kikubwa kutokana na Wachezaji wa TASWA FC kuwa katika hali ya kiwango cha juu kutosha kuwapima Wachezaji hao ambao muda mwingi utumia kuchezea nafasi ya Mlinda Mlango, hivyo kwao pia ni moja ya zoezi kutokana na kwamba watajitambua kuhusu Pumzi pamoja na kujenga Mahusiano Mema kati yao wenyewe, na kutokana na mchezo huo kuwa wa aina yake imetulazimu kumtafuta Mgeni Rasmi ili aje atazame mchezo huo kwani burudani ya leo ni kubwa, na mgeni wetu ni Kamanda Kova"amesema Majuto
Kikosi cha makipa kinatazamiwa kuomngozwa na Ivo Mapunda, Juma Kaseja, Dida, Ally Mstafa, Aishi Manula pamoja na wengine wengi huku kikosi cha Timu ya Waandishi wa Habari (TASWA FC) kinatazamiwa kuongozwa na Kocha Mchezaji Ally Mkongwe, Ibrahim Maestro Masoud, Juma Pinto, Sarehe Ally, Mwidini Sufiani, Mpalule Shaaban, Salum Jaba, na wengine Wengi.
No comments:
Post a Comment