Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa
Bima ya Afya ya Taifa NHIF Bw. Khamis Mdee wa pili kutoka kulia
akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya mfuko huo
wakati walipoonyesha tuzo ambazo mfuko huo ulitunukiwa nchini Morocco na
Shirikisho la kimataifa la Taasisi za Hifadhi ya Jamii (ISSA) nchini Morocco hivi karibuni. kulia ni Mkurugenzi wa Uendeshaji (NHIF),Eugen Mikongoti,
Kutoka kushoto Kaimu Mkurugenzi Tiba na Ushauri wa NHIF, Dk Mkwabi
Fikirini na Mkurugenzi wa masoko na Utafiti NHIF,Raphael Mwamoto wakiwa
katika mkutano huo uliozungumzia tuzo hizo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa
Bima ya Afya ya Taifa NHIF Bw. Khamis Mdee wa pili pamoja na wakurugenzi
wa shirika hilo kulia Mkurugenzi wa Uendeshaji (NHIF),Eugen Mikongoti,
Kutoka kushoto Kaimu Mkurugenzi Tiba na Ushauri wa NHIF, Dk Mkwabi
Fikirini na Mkurugenzi wa masoko na Utafiti NHIF,Raphael Mwamoto
wakionyesha tuzo zilizokabidhiwa kwa mfuko huo kutoka Shirikisho la
kimataifa la Taasisi za Hifadhi ya Jamii (ISSA) nchini Morocco hivi
karibuni
……………………………………………………………………………………………………..
Kwa miaka mingi sasa, Mfuko wa
Taifa wa Bima ya Afya umekuwa mwanachama wa mashirikisho mbalimbali ya
kimataifa ikiwemo Shirikisho la kimataifa la Taasisi za Hifadhi ya Jamii(ISSA),Shirikisho la Hifadhi ya Jamii la Nchi za Afrika Mashariki na
Kati (ECASSA), na Shirikisho la kimataifa la Uchumi wa Afya (IHEA).
Mashirikisho haya husaidia katika kubadilishana uzoefu katika maeneo
mbalimbali, ushauri wa kitaalamu, viwango vya huduma, miongozo ya
kiutendaji pamoja na kutumika kama jukwaa kwa wanachama kujenga na
kuhamasisha mifumo endelevu katika hifadhi ya jamii. Taasisi hizi za
kimataifa vilevile huhusika katika kutoa tuzo kwa Taasisi ambazo
zinafanya vizuri katika ubunifu katika maeneo mbalimbali.
Shirikisho la kimataifa la Taasisi
za Hifadhi ya Jamii(ISSA)limekuwa na utaratibu wa kushindanisha
mifuko ya hifadhi ya jamii duniani kwenye maswala ya ubunifu katika
maeneo mbalimbali ya kiutendaji yakiwemo; kuboresha huduma, utawala
bora, matumizi ya teknolojia, ukusanyaji wa michango na matekelezo,uwekezaji,kufikisha huduma kwa wananchi waliyo sehemu ngumu kufikika,
uhamasishaji wa Afya na uepushaji wa hatari makazini, pamoja na
utekelezaji wa tathmini za uhai wa mifuko. Mashindano haya yalianza
tangu mwaka 2008 na hufanyika kila baada ya miaka mitatu.
Tangu kuanzishwa kwa tuzo hizi,
Mfuko umekuwa ukishinda tuzo katika maeneo mbalimbali. Mwaka 2008 Mfuko
ulishinda tuzo moja ya ubunifu katika kuboresha huduma na mawasiliano
kwa wanachama kupitia siku ya wadau (Clients Days).
Mwaka 2011 Mfuko ulishinda tuzo nne katika masuala yafuatayo;
Uboreshaji wa kitita cha mafao yanayotolewa na Mfuko;Usimamizi wa Mfuko wa Afya ya Jamii: katika kupanua wigo na jitihada za kufikia lengo la afya kwa Watanzania wote; Utoaji wa mikopo ya vifaa tiba na Uboreshaji wa majengo inayotolewa na Mfuko; Ugatuzi wa shughuli za Mfuko kwa kufungua ofisi za mikoa kuwasogezea huduma wananchi: Usimamizi bunifu kuongeza ufanisi katika utendaji. Kwa mara nyingine Mfuko umeshinda tuzo tatu za ubunifu katika sekta ya hifadhi ya Jamii Barani Afrika katika sherehe za kukabidhi tuzo hizo zilizofanyika tarehe 3 Disemba 2014 katika hoteli ya Sheraton mjini Casablanca, Morocco. Tuzo ambazo NHIF ilikabidhiwa ni katika eneo la utoaji wa huduma za matibabu za kibingwa maeneo magumu kufikika, kazi ambayo Mfuko umekuwa ukifanya kwa kushirikiana na wataalamu wa hospitali za rufaa nchini tangu mwaka 2012.

Tuzo nyingine ni katika eneo la
TEHAMA katika utayarishaji pamoja na uwasilishaji wa madai ulioanzishwa
kwa dhumuni la kupunguza malalamiko ya baadhi ya vituo vya Afya
kuchelewa kulipwa madai yao. Kupitia mfumo huu, muda wa ulipaji wa madai
hasa katika hospitali kubwa nchini umepungua kwa kiasi kikubwa sana.
Mfumo huu ulianza tangu Januari 2012.
Tuzo ya tatu ni juu ya huduma za matibabu kwa wanachama wastaafu
ambayo imeanza tangu mwaka 2011. Fao la wastaafu linalenga kuwapa
wananchi ambao walikuwa wanachama wa Mfuko na wenza wao uwezo wa
kutibiwa kupitia Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya baada ya kustaafu ajira
mpaka mwisho wa maisha
Mfuko utaendelea kufuata miongozo
inayotolewa na mashirika ya kimataifa ili kutekeleza shughuli zake
kiufanisi na kuhakikisha unatoa huduma bora kwa wanachama wake.
Mfuko vilevile unadhamiria kuendelea kuboresha shughuli zake ili
uweze kukidhi viwango vya kimataifa vinavyotolewa na Shirika la viwango
la kimataifa (ISO) na hatimaye kuthibitishwa kwa kutimiza viwango hivyo
katika kipindi kifupi kijacho.
NHIF Mfuko pia unatarajia kwa kipindi kijacho kuweza kukidhi
viwango vilivyowekwa na Shirikisho la kimataifa la Mifuko ya Hifadhi ya
Jamii (ISSA) na kupata ithibati ya kukidhi viwango vya kimataifa.
No comments:
Post a Comment