Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
atazungumza na Wazee wa Mkoa wa Dar Es Salaam, mchana wa Jumatatu,
Desemba 22, 2014.
Wakati wa mazungumzo
yake na Wazee hao, Rais Kikwete atazungumzia masuala mbali mbali ya
kitaifa, yakiwemo yale ambayo yamekuwa yanasubiri maamuzi yake tokea
alipokuwa anajiuguza kufuatia upasuaji aliofanyiwa mwezi uliopita,
Novemba 2014.
Undani zaidi kuhusu
mkutano huo kama vile mahali utakapofanyika, saa utakapofanyika na nani
wataalikwa utatolewa na mamlaka zinazohusika na maandalizi ya mkutano
huo.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
19 Desemba, 2014
No comments:
Post a Comment