Katibu
wa chama cha mapinduzi mkoani Iringa HASSAN MTENGA akiongoza makatibu
wa wilaya kuongea na waandishi wa habari mkoani Iringa
………………………………………………………………………………………..
Na Fredy Mgunda,Iringa
Katibu wa chama cha mapinduzi CCM
HASSAN MTENGA amekiri kuhusu sakata la fedha za tegeta ESRWO na IPTL
kuwa limechangia kudondoka katika uchaguzi wa serikali za mitaa
uliofanyika hivi karibuni.
Akizungumza na waandishi wa habari amesema kuwa suala hilo
lilihitaji elimu kubwa kuwaelimisha wananchi kabla ya uchaguzi huo wa
serikali za mitaa.
Mtenga amesema dalili za awali
kuhusu uchaguzi mkuu utakao fanyika mwakani ni nzuri kuhusu chama cha
Mapinduzi na watashinda kwa kishindi kama uchaguzi wa serikali za mitaa.
Aidha amezungumzia kuhusu vijana walioondoka katika chama cha
mapinduzi na kujiunga na Chadema kuwa umetumika ujanja wa kuwa nunua
vijana ili kupigia kura chama cha demokrasia na maendeleo Chadema.
Kwa upande wa chama cha mapinduzi wilayani mufindi mkoani Iringa
wameulalamikia uongozi wa serikali uliopewa dhamana ya kusimamia zoezi
zima la uchaguzi wa serikali za mitaa ambapo dosari nyingi zimejitokeza
tofauti na chaguzi zilizopita.
Akizungunza na na mtandao huu katibu wa chama hicho wilayani
mufindi MIRAJI MTATARU amesema kuwa uchaguzi huu umekuwa na changamoto
nyingi hivyo kupelekea ucheleshaji wa vifaa pamoja na kufanya uchaguzi
kuwa kama wa kushitukiza wakati walikuwa wamejipanga kwa muda muda
mrefu.
MTATURU ameitaka serikali iangalie kwa makini suala hili la
uchaguzi kwa kuwa kuna wananchi wengi wamekosa haki yao ya msingi kwa
kuwa walishindwa kupiga kuwa kutokana na kukosekana kwa karatasi za
kupigia kura.
Aidha MTATURU amewapongeza
wananchi wa wilaya ya mufindi kuendelea kukipigia kura wagombea wa CCM
na kuwapa ushindi wa asilimia 99 na kuwaachia wapinzania asilimia moja
tu licha ya changamoto zilizojitokeza kwenye uchaguzi huo.
No comments:
Post a Comment