Na Mwandishi Wetu
WAKATI Tamasha la Krismasi liko mbioni kufanyika katika mikoa ya Mbeya, Iringa na Ruvuma wilaya ya Songea, Kampuni ya Msama Promotions inayoandaa tamasha hilo imeeleza kwamba waimbaji wengi walioshiriki semina zinazondaliwa na kampuni hiyo kwa kushirikiana Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) wamefanikiwa. Kampuni ya Msama Promotions huandaa semina hizo kwa sababu ya kuwaweka sawa waimbaji kabla ya kupanda jukwaani yakiwemo maadili. Kwa mujibu wa Katibu wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Jimmy Rwehumbiza mbali ya kuwa kuna changamoto ya waimbaji kutohudhuria katika semina hizo, ambao wanahudhuria wanafaidi mbinu mbalimbali pamoja na kujua haki zao. Alisema katika semina hiyo waimbaji wanajifunza mambo mbalimbali ikiwemo mikataba. Rwehumbiza alisema kuwa faida nyingi zimepatikana kupitia semina hizo ambazo zimefanyika kwa muda mfupi ambako waimbaji imewasaidia kujisajili katika Baraza hilo na kutambulika kisheria ili kuwarahisishia mambo mbalimbali yakiwemo safari za nje ya nchi. Mwimbaji wa nyimbo za Injili, Edson Mwasabwite alisema kilio chao kikubwa ni kuibiwa kwa kazi zao huku akiilalamikia Serikali kuwa imewatupa bila kuwasaidia katika kutatua tatizo hilo la wizi unaozidi kila kukicha. Mwimbaji huyo pia aliishukuru kampuni ya Msama Promotions ambayo imekuwa ikifanya kazi kubwa ya kukamata wazalishaji wa kazi feki za wasanii hapa nchini. Basata kupitia Ofisa wake Kwirujira Ng’oko Maregesi, aliwataka waimbaji hao kupitia Chama chao kumtumia mwanasheria wao na kusisitiza waimbaji kusimamia kazi zao na kutambua mikataba yao. Mbali na hayo pia Basata iliwaasa waimbaji kuacha kuuza kazi zao halisi ‘Master’ kwani kufanya hivyo ni kuwatajirisha wanaowauzia wasambazaji, ambako aliwataka waimbaji kuimba kwa kutumia vyombo kwani Watanzania wamechoka na mfumo wa ‘Play back’. Naye mdau aliyepata fursa ya kushiriki semina hiyo John Melele alisema serikali ilaumiwe kwa kushindwa kudhibiti tatizo hilo huku akitoa ushauri kiundwe chombo kitakachoifikia kila Halmashauri ya Mkoa na kuwatumia watendaji watakaoshughulikia masuala hayo huku akisisitiza kuwa kuwaachia waimbaji na msambazaji.
No comments:
Post a Comment