Ofisa
mwandamizi wa habari na mahusiano ya umma wa Taasisi ya Sayansi na
Teknolojia ya Nelson Mandela, Bw. Karimu Meshack (kushoto) akijadiliana
jambo ndani chumba cha mapumziko cha wageni mashuhuri na Mwakilishi
mkazi shirika la UNESCO nchini Bi. Zulmira Rodrigues pamoja na Afisa
mipango kitaifa, kitengo cha Sayansi UNESCO,Tanzania, Gabriela Lucas
kabla ya kuwasili kwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa
Mataifa la Maendeleo ya Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Getachew
Engida.
Mwakilishi mkazi shirika la UNESCO nchini Bi. Zulmira Rodrigues akimlaki Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Getachew Engida
wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro
(KIA) kwa ajili kuhudhuria mahafali ya pili ya Taasisi ya Sayansi na
Teknolojia ya Nelson Mandela jijini Arusha yanayofanyika kesho.
Kulia ni Ofisa mwandamizi wa habari na mahusiano ya umma wa Taasisi ya
Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, Bw. Karimu Meshack na wa pili
Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya UNESCO, Dr. Moshi Kimizi.
Mwakilishi
mkazi shirika la UNESCO nchini Bi. Zulmira Rodrigues (katikati)
akimlaki kwa furaha Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa
la Maendeleo ya Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Getachew Engida
(kushoto) aliyewasili jioni hii jijini Arusha na shirika la ndege la
Ethiopia. Kulia ni Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya UNESCO, Dr.
Moshi Kimizi.
Naibu
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Elimu,
Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Getachew Engida akisalimiana na Ofisa
mwandamizi wa habari na mahusiano ya umma wa Taasisi ya Sayansi na
Teknolojia ya Nelson Mandela, Bw. Karimu Meshack kwenye uwanja wa ndege
wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).
Naibu
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Elimu,
Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Getachew Engida akiwa na mwenyeji wake
Mwakilishi mkazi shirika la UNESCO nchini Bi. Zulmira Rodrigues mara
baada ya kuwasili wakielekea kwenye chumba cha mapumziko cha wageni
mashuhuri.
No comments:
Post a Comment