Mwakilishi
wa kampuni ya Al- Riyamy Production Bakari Kassim almaarufu Mzee
Jangala,(kulia) akimuonyesha stakabadhi ya malipo Katibu Mtendaji wa
Bodi ya Filamu , Joyce Fisoo baada ya kufanya malipo ya kupata kibali
kwa ajili ya filamu za kampuni hiyo,leo jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mtendaji wa Bodi ya Filamu , Joyce Fisoo akiamkabidhi kibali cha filamu
mwakilishi wa kampuni ya Al- Riyamy Production Bakari Kassim almaarufu
Mzee Jangala,(kulia) baada ya kufanya malipo ya filamu zao zote zikiwemo
za zamani na mpya,leo jijini Dar es Salaam.
Afisa
Utamaduni wa Bodi ya Filamu Clarence Chelesi(kulia) akimpa mkono wa
pongezi mwakilishi wa kampuni ya Al- Riyamy Production Bakari Kassim
almaarufu Mzee Jangala,(kushoto) baada ya kupata kibali cha filamu,leo
jijini Dar es Salaam.
Afisa
Utamaduni wa Bodi ya Filamu Simon Peter (kulia) akimpa mkono wa pongezi
mwakilishi wa kampuni ya Al- Riyamy Production Bakari Kassim almaarufu
Mzee Jangala,(kushoto) baada ya kupata kibali cha filamu wanaotazama ni
Afisa Utamaduni wa Bodi ya Filamu Clarence Chelesi(katikati) na Katibu
Mtendaji wa Bodi ya Filamu , Joyce Fisoo (kushoto) ,leo jijini Dar es
Salaam.(Picha zote na Lorietha Laurence-Maelezo)
………………………………………………………………………….
Lorietha Laurence -Maelezo
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu , Joyce Fisoo ametoa wito kwa
kampuni za Filamu nchini kuwasilisha filamu zao ili ziweze kuhakikiwa na
kulipiwa kwa kupata kibali cha kuingia sokoni kama sheria ya filamu ya
mwaka 1976 kifungu namba 4 inavyoeleza.
Akizungumza katika ofisi za Bodi leo jijini Dar es Salaam, Fisoo
ameipongeza kampuni ya Al-Riyamy Production ambayo imeweza kutimiza
wajibu wake na kulipia filamu 134 ambazo zimepata kibali cha kupatiwa
stamp za TRA na hivyo kuwa tayari kuingia sokoni.
Aliongeza kuwa kuna baadhi za kampuni za filamu nchini zimekiuka
utaratibu na kushindwa kuwasilisha filamu zao kwa Bodi ikiwemo filamu
zile zilizoigizwa miaka ya zamani ambazo zimekuwa zikionyeshwa bila
kibali.
“Nimefurahishwa sana kwa namna ambavyo kampuni ya Al-Riyamy
Production kwa kufuata sheria na kanuni za filamu nchini, hivyo natoa
wito kwa kampuni nyingine pia kuweza kufanya hivyo ili kukuza uchumi
wetu na wao waweze kufanya biashara bila usumbufu” alisema Fisoo
Naye mwakilishi wa kampuni ya Al- Riyamy Production Bakari
Kassim almaarufu Mzee Jangala, amewaomba wasanii wenzake wenye kampuni
za filamu waweze kufuata taratibu na sheria za bodi ya filamu ili kukuza
soka la filamu na kuinua uchumi wa nchi yetu.
“Nawasiii wasanii wenzangu na wamiliki wa kampuni za filamu
nchini waweze kufuata sheria na kanuni za filamu ili tuweze kwenda
vizuri kwa kila mmoja kutimiza wajibu wake katika ulimwengu huu wa
filamu” alisema Mzee Jangala.
Baadhi ya kampuni ambazo zimeweza kuwasilisha kazi zao katika
Bodi ya filamu ,ni pamoja na kampuni ya Wananchi wote wamewasilisha
filamu 119, Game First Quality filamu 35, steps Entertainment filamu
739, na Al-Riyamy Production filamu 134.
No comments:
Post a Comment