Washiriki
wa kikao kazi cha kuandaa miongozo (checklist) ya ukaguzi wa migodi
wakiwa katika makundi kujadiliana namna ya kuandaa miongozo hiyo.
Mtaalamu
kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Idara ya Madini, Mhandisi Noel
Baraka akiongea jambo wakati akitoa mada kuhusu Ukaguzi wa Madini wakati
wa kikao kazi cha Wakaguzi wa Migodi nchini.
Baadhi
ya washiriki wa kikao kazi cha kuandaa checklist ya wakaguzi wa migodi
wakiwa katika kazi za vikundi kuandaa miongozo hiyo.
………………………………………………………………………
Na: Asteria Muhozya, Mwanza
Imeelezwa kuwa, wakaguzi wa migodi wanao mchango mkubwa katika
kuepusha ajali zinazotokea migodini hususani kwa wachimbaji wadogo
endapo watatoa mapendekezo na maoni yatakayowezesha kuandaa miongozo
(checklist) itakayotumika katika ukaguzi wa migodi.
Hayo yameelezewa na Mtaalamu kutoka Idara ya Madini, Wizara ya
Nishati na Madini , Mhandisi Noel Baraka wakati akitoa mada katika kikao
kazi cha wakaguzi wa migodi wanaokutana kwa lengo la kuandaa checklist
zitakazotumika kwa ajili ya shughuli za ukaguzi wa migodi.
Akizungumzaia hali halisi ya watalaamu hao, alieleza kuwa, bado
kuna upungufu wa wakaguzi wa migodi huku idadi kubwa ikiwa ni watalaamu
wachanga ambao bado hawana uzoefu wa kutosha katika shughuli hizo.
“Pamoja na upungufu huu lakini endapo tutaandaa checklist nzuri
itasaidia kwa kiasi kikubwa kuepusha ajali migodini,” ,alisisitiza
Baraka.
Wakati huo huo, akitoa mada katika kikao hicho, Mhandisi Assa
Mwakilembe amewataka wakaguzi hao kuzingatia maeneo muhimu mbalimbali
ambayo yameainishwa katika Sheria ya Madini ya mwaka 2010 yakiwemo
masuala ya uhifadhi wa mazingira, usalama na afya na kuwataka wataalamu
hao kutoa kipaumbele katika maeneo hayo wakati wa shughuli za ukaguzi wa
migodi nchini.
Vilevile, akitoa mada ya namna ya kuandaa miongozo ya ukaguzi
(checklist), Kamishna Msaidizi anayeshughulikia Ukaguzi wa Migodi
Mhandisi Ally Samaje ameeeleza umuhimu wa kuwa na checklist katika
shughuli za migodi kwamba, zitawezesha kufahamu mapungufu yaliyoko
migodini na hivyo kujua namna bora ya kutoa ushauri wafanyapo ukaguzi
katika migodi ya wachimbaji wakubwa na wadogo.
No comments:
Post a Comment