Sehemu ya Washiriki wa semina ya
mabadiliko ya Tabia Nchi inayofanyika mjini Morogoro. Semina hiyo
imeandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais.
…………………………………………………………………………..
Wito umetolewa kwa kila Mwananchi
kushiriki katika utekelezaji wa mkakati wa tabianchi ili kuweza kupata
maendelo endelevu. Pia kuhakikisha utunzaji wa mazingira unapewa
kipaumbele. Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Sazi
Salula wakati wa ufunguzi wa semina ya mabadiliko ya tabianchi
iliyofanyika mjini Morogoro.
Aliongeza kuwa semina hiyo itaongeza uelewa kuhusu juhudi
zinazohitajika katika kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi katika
jamii za maeneo ya Pwani. “Mabadiliko ya tabianchi kwa siku zijazo
yanaweza kusababisha gharama kubwa za kiuchumi pia kuathiri mamilioni ya
maisha ya watu” alisema Bwana Salula.
Akimkaribisha Mgeni Rasmi Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya
Makamu wa Rais Bwana Julius Ningu amewataka Wadau walioshiriki semina
hiyo kuendelea kuongeza nguvu ili kuweza kukabiliana na mabadiliko ya
tabia nchi. Alisema kuwa ni jukumu la kila mmoja kusimamia hilo.
Aidha aliwashukuru washiriki kwa kuhudhuria na kuwaomba wakawe
mfano kwa wengine katika kutoa elimu ya mabadiliko ya tabianchi ili
kuweze kutokomeza janaga hilo.
No comments:
Post a Comment