MWENYEKITI wa klabu ya Yanga
Yusuph Manji ameitangaza Sekretarieti mpya ya Uongozi katika Klabu hiyo
yenye Maskani Mtaa wa Jangwani Jijini Dar Es Salaam.
Sektretarieti hiyo ambayo
itaongozwa na Katibu Mkuu Dk Jonas B Tiboroha ambae atafanya kazi na
Mkuu wa Idara ya habari na Mawasialiano bwana Jerry Cornel Muro,Bwana
Omar Kaya yeye anakuwa Mkuu wa Idara ya masoko
Wengineo ni Bwana Frank Chacha anakuwa Mkuu wa Idara ya Sheria pamoja na bwana Charles Boniface ambae atakuwa Kocha Msaidizi
Akithibitisha Kuteuliwa kwa
Viongozi hao wajuu Klabuni hapo mda huu Jijini Dar Es Salaam wakati wa
Mkutano na Waandishi wa Habari na Mkuu wa Idara ya habari na
Mawasialiano bwana jerry Cornel Muro pamoja na kutangaza Viongozi hao
wapya alisema
Wanachama,Mashabiki,Wapen pamoja
na wapenzi wa Klabu hiyo washirikiane na Viongozi hao wapya kuiletea
maendeleo Klabu hiyo kubwa nchini.
Aidha,jery Murro alisema
Mwenyekiti wa yanga anamshukuru sana Bwana aliyekuwa kocha mkuu wa timu
hiyo mbrazili MARCIO MAXIMO pamoja na msaidizi wake kwa ushirikiano wo
waliouonyesha katika timu hiyo na kuwatakia heri katika maisha yao huko
waendako.
Katika hatua nyingine amesema kuwa
yanga imeamua kuongeza vijana katika uongozi wake ili muda wa kustaafu
ukifika yanga iyakuwa na waridhi bora watakaoendeleza mazuri
waliyoyakuta..
No comments:
Post a Comment