15 KUTOKA NJE WAOMBEWA USAJILI DIRISHA DOGO
Usajili wa dirisho dogo msimu
wa 2014/2015 umefungwa jana (Desemba 15 mwaka huu) huku wachezaji 15
kutoka nje wakiombewa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kutoka nchi
mbalimbali.
Wachezaji walioombewa ITC kwa timu
za Ligi Kuu ni Abdulhalim Humoud kutoka Sofapaka ya Kenya kwenda
Coastal Union, Brian Majwega kutoka KCC (Uganda) kwenda Azam, Castory
Mumbara kutoka Three Star Club (Nepal) kwenda Polisi Mara, Charles
Misheto kutoka SP Selbitiz (Ujerumani) kwenda Stand United na Chinedu
Michael Nwankwoeze kutoka Nigeria kwenda Stand United.
Dan Serunkuma kutoka Gor Mahia
(Kenya) kwenda Simba, Emerson De Oliveira Neves Roque kutoka Emerson De
Oliveira Neves Roque kutoka Bonsucesso FC (Brasil) kwenda Yanga, Halidi
Suleiman kutoka Flambeau (Burundi) kwenda Stand United na Juuko Murushid
kutoka SC Victoria University (Uganda) kwenda Simba.
Kpah Sean Sherman kutoka Aries FC
(Liberia) kwenda Yanga, Meshack Abel kutoka KCB (Kenya) kwenda Polisi
Morogoro, Moussa Omar kutoka Flambeau (Burundi) kwenda Stand United,
Nduwimana Michel kutoka Flambeau (Burundi) kwenda Stand United, Serge
Pascal Wawa kutoka El Merreikh (Sudan) kwenda Azam na Simon Serunkuma
kutoka Express FC (Uganda) kwenda Simba.
Kamati ya Sheria na Hadhi za
Wachezaji ya TFF inatarajia kukutana hivi karibuni kwa ajili ya kupitia
usajili wa wachezaji wote walioombewa katika dirisha dogo wakiwemo wale
wa mkopo.
RAMBIRAMBI MSIBA WA KOCHA MADEGA Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Kocha
Mshindo Madega kilichotokea leo (Desemba 16 mwaka huu) mjini Bukoba.
Mbali ya kuwahi kuwa mchezaji
katika timu ya RTC Kagera, Kocha Madega aliwahi kufundisha timu za
Kagera Stars, Mwadui na kombaini ya Copa Coca-Cola ya Mkoa wa Kagera.
Mchango wake katika mchezo wa mpira wa miguu tangu akiwa kocha na baadaye kocha utakumbukwa daima.
Tunatoa salama za rambirambi kwa
familia ya marehemu, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Kagera (KRFA),
Chama cha Makocha wa Mpira wa Miguu Tanzania (TAFCA) Mkoa wa Kagera na
klabu ya Bukoba Veterans na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika
kipindi hiki kigumu cha msiba huo.
TFF itawakilishwa kwenye msiba huo na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Kagera (KRFA).
MICHUANO YA COPA COCA-COLA YAENDELEA KUTIMUA VUMBI
Michuano ya Copa Coca-Cola kwa
vijana wenye umri chini ya miaka 15 ngazi ya Taifa inaendelea leo jioni
(Desemba 16 mwaka huu) kwa mechi mbili zitakazochezwa jijini Dar es
Salaam na mkoani Pwani.
Uwanja wa Nyumbu uliopo mkoani
Pwani utazikutanisha timu za Mjini Magharibi na Dodoma katika mechi ya
kundi B, wakati kundi C kutakuwa na mechi kati ya Arusha na Mwanza
itakayochezwa Uwanja wa Tanganyika Packers uliopo Kawe jijini Dar es
Salaam.
Wakati kesho (Desemba 17 mwaka
huu) ikiwa ni mapumziko, michuano hiyo itaingia hatua ya robo fainali
keshokutwa (Desemba 18 mwaka huu) kwenye viwanja hivyo hivyo.
No comments:
Post a Comment