(Picha Zote Na: Said Mkabakuli)
……………………………………………………………………………….
Na:Saidi Mkabakuli, Kagera
Kiwanja cha Sukari cha Kagera
kimeanza kuzalisha ziada ya sukari inayohitajika katika soko la sukari
nchini hali inayopelekea kuweza kupunguza tatizo la upatikanaji wa
sukari Tanzania na nchi za jirani zinazotumia sukari kutoka kiwandani
hapo.
Hayo yamewekwa wazi na Meneja Mkuu
wa Kiwanda hicho, Bw. Ashwin Rana, wakati alipokuwa akizungumza na Timu
ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya
Mipango.
“Kwa sasa tumeweza kuongeza mauzo
katika kanda kufikia tani 40,000, pamoja na kuongeza ununuzi kutoka kwa
wakulima wa miwa wa nje zaidi ya tani 100,000 kwa mwaka,” alisema.
Bw. Rana aliongeza kuwa Kiwanda
chake kimewekeza zaidi katika upanuzi wa eneo la shamba la miwa la
umwagiliaji la hekta 3600 pamoja na kuwekeza zaidi katika teknolojia ya
kisasa katika kilimo.
“Kampuni yetu imewekeza kwa kiasi
kikubwa katika teknolojia na vifaa vya kisasa ikiwemo matrekta
yanayotumia setalaiti katika ufanyaji kazi wake katika kuandaa
mashamba,” aliongeza.
Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa
Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence
Mwanri amekipongeza Kiwanda hicho kwa kuwekeza kwenye uzalishaji wa
kisasa wa miwa hali inayoongeza uzalishaji wa sukari kuwa mkubwa
kiwandani hapo.
Bibi Mwanri ameongeza kuwa Kiwanda
hicho kinastahili pongezi za kipekee kwa kuweza kuongeza ajira zaidi ya
watu 6000 waliopo kiwandani.
“Kwa kweli munastahili sifa kwa kutoa ajira kwa vijana wa Kitanzania pamoja na kuuza umeme kwenye gridi ya Taifa,” alisema.
Kwa mujibu wa Meneja wa Kiwanda
hicho, kwa sasa kinakabiliwa na na changamoto za uuzaji haramu wa sukari
zinazoingia kimagendo nchini ambao umechangiwa kushindwa kwa kiwanda
kuuza sukari ili kurudisha gharama za uzalishaji kutokana bei za sukari
zinazoagiwa kutoka nje kuwa bei ya chini sana.
“Bei ya Sukari Duniani imeshuka
sana kutokana na Nchi kubwa duniani kusaidia wakulima katika uzalishaji
na pembejeo (subsidies) na hivyo sukari kuuzwa katika soko la dunia kwa
bei ya chini (Dumping) na kufanya kuwa bei kuwa ndogo kuliko gharama
halisi ya uzalishaji,” aliongeza.
Aliongeza kuwa changamoto nyingine
ni pamoja na kiwanda kushindwa kulipa mikopo iliyochokuwa benki
kutokana na kuwepo sokoni kwa sukari ambayo ni ya magendo na bei ya
chini hivyo kiwanda kushindwa kufikia malengo hata ya kiundeshaji na
mipango mikakati.
Kiwanda cha Sukari cha Kagera kiko
katika sehemu Kaskazini Magharibi ya Tanzania (karibu na mpaka wa
Tanzania na Uganda) kilibinafsishwa na Serikali kwa sekta binafsi mwaka
2001. Malengo ya ubinafsishaji yalikuwa kuboresha upanuzi wa masoko ya
ndani na kikanda, uwekezaji wa kisasa, upanuzi na ukarabati na majengo
ili kuhakikisha shughuli za kiundeshaji zinaboreshwa.
No comments:
Post a Comment