Maafisa, Wakaguzi, na Askari wa
Jeshi la Polisi hapa nchini, wametakiwa kudunisha nidhamu wakati wote,
kutenda haki kwa kila mmoja na kuwaheshimu wananchi wa rika zote bila ya
kujali dini, rangi ama itikadi zao kisiasa.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Chuo cha Polisi Dar es Salaam, SACP Ali Lugendo, wakati akizungumza na Wanafunzi wa Mafunzo ya Uofisa (Mrakibu Msaidiizi wa Polisi) na wale wa cheti na Stashahadi ya Sayansi ya Polisi kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini.
Kamanda Lugendo amesema kuwa
pamoja na kufundisha masomo ya sheria na haki za binadamu, lakini kazi
kubwa inayofanywa na chuo chake ni kusisitiza nidhamu kwa kila afisa na
askari wanaofika chuoni hapo.
Amesema kuwa nidhamu ni somo la
kwanza analofundishwa askari anapokuwa katika mafunzo ya awali kwenye
chuo cha Polisi Moshi kwani amesema nidhamu ni msingi wa kwanza kwa
majeshi yote duniani.
“Hakuna Jeshi lolote duniani,
likiwemo Jeshi letu la Polisi hapa nchini ambalo haliendeshi kwa misingi
ya nidhamu”. Alisema Kamanda Lugendo na kuongeza kuwa bila nidhamu
hakuna Jjeshi.
Kwa upande wake, Afisa Mkuu wa Nidhamu kwenye chuo cha Polisi Dar es Salaam (Dar es Salaam Police Academy)
SSP Mussa Loyd, aliwataka Maafisa hao kuwa kioo cha jamii na kuwatendea
haki wananchi bila ya upendeleo wakati wote wanapokuwa kazini katika
maeneo mbalimbali.
Alisema kuwa, mbali ya kuzuia
vitendo vya kuhalifu, kushuku, kupeleleza na kuwakamata watuhumiwa,
lakini kazi kubwa ya Jeshi la Polisi ni kuhakikisha kuwa kila Askari
anatenda haki kwa kila anayemhudumia bila ya ubaguzi ama kumuonea mmoja
wao.
“tunachotakiwa kufanya sisi
Polisi ni kutenda haki kwa kila mmoja bila ya kujali dini, kabila, rangi
ama itikadi ya mwananchi kisiyasa maana sisi hatuna chama”. Alisema
Loyd.
No comments:
Post a Comment