Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (wanne Kushoto) akifuatilia kwa
umakini mazungumzo kwa njia ya mtandao na watu wa Kenya, alipotembelea
ofisi ya Wakala wa Mafunzo kwa njia ya mtandao (TaGLa), jijini Dar es
Salaam.
Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (wanne Kushoto) akifuatilia kwa
umakini mazungumzo kwa njia ya mtandao na watu wa Kenya, alipotembelea
ofisi ya Wakala wa Mafunzo kwa njia ya mtandao (TaGLa),leo jijini Dar es
Salaam.
Wajumbe
wa bodi ya Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao(TaGLa) wakifuatilia
mazungunzo kwa njia ya mtandao na watu wa Kenya, Mafunzo kwa njia ya
mtandao (TaGLa),leo jijini Dar es Salaam
Menaja
wa tecknolojia TaGLA ,Bwana Emmanuel Tessua wa kwanza kushoto, akitoa
maelekezo kwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (wa pili kulia)
ya namana mikutano inavyofanyika kwa kutumia mtandao katika chumba cha
mikutano wakati wa Ziara yake leo jijini dare s Salaam , wa kwanza kulia
ni Mkurugenzi Mtendaji wa TaGLA Bwana Charles Senkondoleo jijini Dar es
Salaam.
Mkurugenzi
Mtendaji wa TaGLA Bwana Charles Senkondo akitoa maelekezo kwa Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika kituo cha taarifa za
maendeleo(TDIC) alipotembelea ofisi hizo leo jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue ( wa tatu kushoto) akiangalia namna
majadiliano yanavyofanyika kwa mfumo wa kutumia mtandao katika ofisi za
Wakala wa Mafunzo kwa njia ya mtandao (TaGLa) wakati wa ziara yake leo
jijini Dare s Salaam, wa kwanza kushoto ni Menaja wa tecknolojia TaGLA
,Bwana Emmanuel Tessua na wa pili ni Mkurugenzi Mtendaji wa TaGLA Bwana
Charles Senkondo.
………………………………………………………………………………
Na Lorietha Laurence- MAELEZO
Serikali imejidhatiti katika
kuboresha huduma za mawasilano kwa Njia ya Mtandao (TEHAMA) ili
kurahisisha utendaji wa shughuli mbalimbali za kiserikali.
Akiongea na wajumbe wa bodi ya Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya
Mtandao (TaGLA), jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi
Ombeni Sefue amesema lengo la Serikali ni kuongeza ufanisi kwa watumishi
na jamii kwa ujumla kujifunza na kuwasilisha mada mbalimbali kupitia
mtandao.
Balozi Sefua amesema kuwa serikali na taasisi zake mbalimbali
hazina budi kutumia wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao kufanya
shughuli zake zote zinazotekelezeka kwa njia ya Videoconference na
Mafunzo ya Masafa ili kupunguza gharama.
“Lengo kuu la Serikali ni kurahisisha mawasilino baina ya
watumishi na jamii ili kupunguza usumbufu wa safari ndefu kutoka sehemu
moja kwenda nyingine na pia kuokoa muda, na urahisi wa upatikanaji wa
huduma kwa wananchi” alisema.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Mafunzo kwa
Njia ya Mtandao (TaGLA), Bwana Charles Sekondo, amesema ofisi yake
imekuwa ikitekeleza majukumu kwa ufanisi kwa kushirikiana na wadau
mbalimbali wanaojihusisha na mafunzo kwa njia ya mtandao ili kwenda
sambamba na maendeleo ya teknolojia duniani katika utekelezaji wa
shughuli mbalimbali za kijamii na kiserikali.
“Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao imerahisisha sana
mawasiliano baina ya serikali, wizara, idara , wakala wa Serikali,
pamoja na Sekta binafsi katika kuboresha uweledi kiutendaji kupitia
utawala bora, anuai za jamii, maswala ya afya na mazingira” alisema
Sekondo
Katika Ziara hiyo Katibu Mkuu Kiongozi alitembelea maeneo
mbalimbali ya ofisi ya Wakala wa Mafunzo kwa njia ya Mtandao ikiwemo
Sehumu ya Huduma za Video Conference, Chumba cha Maabara za Kompyuta na
kituo cha taarifa za maendeleo (TDCI).
Mtandao wa TaGLA,unajukumu la kuwajengea uwezo watumishi wa
wizara, idara na wakala wa serikali pamoja na sekta binafsi katika
nyanja mbalimbali ikiwemo , mafunzo ya midahalo kwa njia ya video ya
hapa nchini na nchi nyingine, midahalo kwa njia ya mtandao, mafunzo ya
ana kwa ana na mafunzo kwa njia ya uongozi.
No comments:
Post a Comment